Ameandika Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire "Nawashukuru, nawapongeza sana wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, wapenzi, wadau, mashabiki wa Ruvu Shooting FC na Simba SC, kadharika Watanzania wote Wazalendo, kwa kufanya vyema katika michezo yao iliyochezwa Februari 20, 2022, timu zote zikiwa ugenini. Ruvu Shooting ikicheza na Tanzania Prisons, ligi ya NBC, uwanja wa Sokoine, Mbeya, ikashinda goli 0-1 dhidi ya Tanzania Prisons, imetoka nafasi ya 15 ya msimamo hadi ya 12. Simba SC, wakicheza hatua ya makundi, kombe la Shirikisho Afrika na timu ya USGN huko Niger, iliwalazimisha wenyeji hao sare ya goli 1-1, matokeo ambayo yameifanya iongoze kundi kwa pointi 4. Watanzania wazalendo, tuendelee kuiombea Simba SC, iendelee kufanya vizuri katika michezo ijayo ya mashindano hayo ya Shirikisho Afrika, ili izidi kuitangaza nchi kiuchumi, lakini pia zaidi sana katika ubora wa soka. Wengi walidhani Ruvu Shooting ni timu dhaifu ilipofungwa na Simba SC magoli 7-0, bila kujua ilikuwa ikip...