IBENGE: TUTAWATULIZA MORRISON NA SAKHO

 IBENGE: TUTAWATULIZA MORRISON NA SAKHO


Kocha wa Berkane, Mkongomani Florent Ibenge amefunguka kuwa kikosi chake kina mtihani mkubwa kuanza kutafuta dawa ya kuwatafutia tiba viungo washambuliaji wawili wa wekundu wa Msimbazi, Pape Sakho na Bernard Morrison ndio mastaa wawili wanaotakiwa kutafutiwa tiba ya kuwatuliza wakati huu beki yao imekuwa na makosa makubwa.

.

“Simba ni timu kubwa, tunakabiliwa na mchezo mgumu dhidi yao, ukiangalia katika mechi zao mbili kuna watu ambao kama tunataka kushinda lazima tuwatafutie mbinu za kuwatuliza,” amesema Ibenge.

.

“Sakho (Pape) ni mchezaji mwepesi anayehitajika kuangaliwa sana kwa jinsi taarifa za mechi zao nilivyozipata lakini kuna yule Morrison (Bernard) ni mchezaji mzuri mwenye ubora akiwa uwanjani achilia mbali nidhamu yake, namjua vyema ni lazima tuwe na akili ya kuwazuia.

.

“Shida yetu ni makosa ambayo mabeki wangu wameyafanya kwenye mechi hizi mbili ni lazima tujue kucheza kwa utulivu kabla ya kukutana na Simba makosa haya ndio yametufikisha hapa kwa hizi mechi mbili,” amesema Ibenge.


Comments

Popular posts from this blog

Shafii Dauda Nipo Huru Sijafungiwa Na TFF

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes