Wanawake Mpo Hii Ni Hatari Sana
HII NI HATARI
Kuna ugonjwa unaitwa gangrene, husababishwa na kukosekana au kutofika kwa damu kwenye sehemu fulani ya mwili.
Damu hukosekana kwa sababu nyingi, ikiwemo kubanwa kwa mishipa ya usambazaji kutokana na uvaaji wa viatu kama hivi.
Mishipa inayosambaza damu mwilini ikibanwa sana, inashindwa kufikisha damu katika maeneo yaliyobanwa.
Damu inapofika sehemu mbalimbali za mwili, husambaza hewa ya oksijeni na virutubisho muhimu kwa afya ya binadamu.
Pia huupatia mfumo wa kinga mwilini viatilifu (antibodies) kusaidia kupambana na maambukizi ya maradhi mbalimbali.
Damu inaposhindwa kusambaa vizuri mwilini, seli za eneo husika haziwezi kuendelea kuwa hai na tishu za sehemu hiyo huoza.
Kuoza kwa tishu za eneo lililoathirika husababisha kubadilika rangi na kuwa ya zambarau, kahawia, bluu au nyeusi.
Gangrene ni ugomjwa hatari sana !
Comments
Post a Comment