Yalipo Mafanikio Ya Simba Sc Yupo Shomari Kapombe

 Unapozungumzia mafanikio ya Simba SC kwa miaka ya hivi Karibuni lazima utaje jina la Shomari Kapombe, Enock  Bwigane alimbatiza jina la "Show me the way".


Nyota huyu aliyekuzwa katika nyumba ya vipaji ya Moro kids pale Morogoro, ni moja ya mabeki Bora kabisa wa upande wa kulia kuwahi kutokea Afrika Mashariki kwa kizazi hiki cha sasa.


Shomari Kapombe sifa yake kubwa ni kuwa na mapafu ya mbwa,  akipandisha mashambulizi kwa kasi kubwa na kurudi kuzuia kwa wakati,  kila Wapinzani wanapolishambulia lango la Simba SC.Hali hii imemfanya awe kipenzi cha mashabiki wa Soka hapa Nchini.


Kama haitoshi Kapombe hajui kuzuia tu bali pia ana uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mwisho kwa washambuliaji ili wafunge na yeye akipata nafasi huweka Mpira kimiani bila ajizi. 


Hii inamfanya awe Beki wa kulia wa  kisasa kabisa kwa sasa huku akilinganishwa sifa zake na Kyle Walker nyota  wa Man City aliyebora  wakati wa kuzuia na pia ni hatari wakati wa kutengeneza shambulizi, hizi ndio sifa za Kapombe " Show me the Way".


Kilichonivutia zaidi msimu huu Kapombe  Kawa moja ya wachezaji hatari na wanaofanya vema katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo hadi sasa amehusika katika Mabao matatu akifunga bao moja na kupiga pasi za mwisho mbili na kuwa mmoja wa mabeki Bora wa kulia wanaofanya vema katika michuano hii ya CAF CONFEDERATION CUP inayoendelea kutimua vumbi huku Simba SC wakiwa wawakilishi pekee kwa upande wa Afrika Mashariki.


Nina Amini nyota huyu ataendelea kufanya vema katika michuano hii ya Kimataifa akiwa na Klabu yake ili mwisho wa msimu awe moja ya mabeki Bora wa Pembeni waliofanya vizuri katika michuano hii kwa sababu ameonyesha mwanzo mzuri, hivyo naamini atakuwa na mwendelezo Bora katika Mechi zinazofuata na ataendelea kuboresha kiwango chake zaidi kwa kadri muda unavyosonga. 


Kila la kheri "Show me the way"  wewe ni mwamba na umwamba wako umejidhihirisha kwa  miaka 10 sasa, hakika umefanikiwa kujitunza na kuwa mpya kila siku.


Vijana wengi sana wanajifunza kutoka kwako wewe ndiye Beki Bora zaidi wa Pembeni ( kulia)  kwa upande wangu na Ubora wako umeuonyesha kwa misimu mingi mtawalia na bado unatuonyesha 🔥🔥. 


@simbasctanzania


  #bwiganetv_soka


Comments

Popular posts from this blog

Shafii Dauda Nipo Huru Sijafungiwa Na TFF

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes