Masau Bwire Watanzania tuiombee ushindi Simba SC
ANAANDIKA MASAU BWIRE.
*Watanzania tuiombee ushindi Simba SC*...
Leo ni siku muhimu sana kwa ustawi wa Simba SC katika mashindano ya Shirikisho Afrika.
Matokeo chanya katika mchezo huo wa ugenini, yataongeza chachu na morari kwa wachezaji, viongozi, mashabiki, wanachama wa Simba SC na Watanzania wazalendo katika kuifikisha timu hiyo hatua nyingine ya robo fainali ya mashindano hayo.
Kufanikiwa kwa Simba SC na kufikia hatua ya juu ya mashindano hayo, ni heshima kubwa mno kwa Simba SC, lakini ni heshima ya kipekee sana kwa nchi yetu kwa maendeleo ya soka letu.
Kwa hali hiyo, niwaombe Watanzania wenzangu wote, tuache tofauti zetu, tuiombee Simba SC ifanye vyema katika mchezo wa leo Jumapili, February 20, 2022, ipate ushindi ugenini, huko Niger dhidi ya USGN.
Lakini pia niwaombe, kwa moyo wa kipekee kabisa, tuiombee Ruvu Shooting, katika mchezo wake wa leo, wa ligi kuu ya NBC, dhidi ya Tanzania Prisons, Sokoine, Mbeya, iweze kuibuka na ushindi.
*Mafanikio ya Simba SC katika mashindano hayo, ni mafanikio ya Tanzania*.
Mungu ibariki Tanzania.
Comments
Post a Comment