LEVY Vs CONTE
LEVY Vs CONTE
Daniel Levy alimpata Mauricio Pochettino ambaye aliikuta Spurs ambayo ipo dhofu bin hali, Muargentina huyo akaibadilisha Spurs bila kutumia pesa nyingi mpaka kuwa timu ya Top 4 na ilikaribia kutwaa taji la EPL ( Mwaka ambao Leicester alikuwa bingwa ) akimaliza nafasi ya 3
- Ilifika wakati Net Spend ya Spurs ilikuwa Pauni Milioni 38 ( Yani ulichotumia na ulichoingiza tofauti yake kwenye usajili ) ni hela ndogo sana tofauti na ilivyokuwa dhidi ya City Liverpool United Chelsea na Arsenal lakini bado Spurs walikuwa Top kwao ipo chini ya Pochettino .
Levy mkono wake wa birika alishindwa kumuunga mkono Pochettino , mwaka 2018 dirisha la usajili la majira ya kiangazi Spurs hawakusajili hata mchezaji mmoja na bado walifika fainali ya UCL 2018/2019.
Akaja Jose Mourinho , kocha ambaye anapenda wachezaji ambao tayari wameiva ili akupe makombe ( amefanya hivyo vilabu vingi ) lakini hadithi ilikuwa ile ile , Spurs waliamua kusajili wachezaji wa bei chee sana na ambao uwezo wao wa kawaida tu .
Akaja Nuno Santo , kama kawaida ya Daniel Levy
Sasa ni zamu ya Antonio Conte , jana baada ya kichapo dhidi ya Burnley Conte alitoa " POVU " kubwa sana kuhusu nia na matamanio ya klabu kama yanalingana na yake
Anaamini klabu inatakiwa kufanya tathimini kwake na kwa klabu yote pia , yeye hapendi kupoteza sana mechi, katika mechi 5 zilizopita, 4 kapoteza ...ukweli ni kwamba anaamini kuna wachezaji hawana ubora unaostahili kushindana na wakubwa zaidi.
Nini anachotaka Levy ??? ANTONIO CONTE ni kocha wa daraja la juu sana na sidhani kama atakubali kuwa katika hali hii ....So , Levy either amuunge mkono Conte mwisho wa msimu huu au mwamba ataondoka huyo
Aliondoka Inter Milan baada ya kuambiwa baadhi ya wachezaji muhimu watauzwa wakati yeye alitaka kuimarisha zaidi ili kutetea taji Serie A na kufanya vizuri UCL . ( Lukaku akapigwa kweli bei, Hakimi akauzwa naye ).
Comments
Post a Comment