Ni Kocha Wa Simba Sc Pablo Vs Kocha Wa ZamalekPatrice Carteron

 ✍️ Pichani ni Kocha wa Simba Pablo Franco 🇪🇦 akiongea na Kocha wa Zamalek Patrice Carteron 🇫🇷 Jana jioni kabla ya mazoezi ya Simba.


♦️Kuna eneo Simba wako bora sana...

Wana mahusiano mazuri na vilabu vikubwa na wana watu sahihi sana wa Logistics


♦️Ni kwakuwa tumechagua kuwadharau Simba Sc...ila Simba kwa sasa ina jina kubwa sana nje ya mipaka ya Nchi.

Natamani timu zingine kama Yanga, Azam na kina Namungo wajifunze kwa Simba Sc.


♦️Ni nadra sana kuona yale yaliyowakuta Namungo pale Angola,Azam kule Swaziland ama Yanga walipokuwa Nigeria yakiwakuta Simba Sc. 


♦️Sikiliza...wale kina Victorien Adebayor na Wilfred Gbeuli wa USGN walikiri wao kwa nyakati tofauti kuwa Simba ni timu kubwa.


♦️Mara kadhaa waandishi wakubwa Afrika kama Lorenz Kohler na Nuhu Adams wamekuwa wakitoa takwimu za ukubwa wa Simba ambazo sisi wabongo wenyewe sometimes tunazikataa.


♦️Hata taarifa zilizosambaa kuwa Simba walilala Airport ni kwa vile tu wabongo tuna utamaduni wa kuzungumza tusiyoyajua


♦️Simba hakwenda Uturuki kufanya Shopping au kuzurura...Simba alikua anatoka Niger kwenda Morocco Via Uturuki yaani ni sawa nawewe unatoka Dar kwenda Tabora kwa kupitia Mwanza umefika Mwanza saa 12 jioni ukaambiwa ndege ya kwenda Tabora itaondoka saa 4 Usiku utaenda kutafuta Hotel mjini au utacheza game mpaka saa 4? Simple tu.


Tukubaliane kuwa Simba inatuwakilisha vyema sana nje ya mipaka ya Tanzania


Sio lazima unielewe leo..


Comments

Popular posts from this blog

Shafii Dauda Nipo Huru Sijafungiwa Na TFF

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes