MASHABIKI 50 WAKWANZA KUCHANJA KUSHUHUDIA MECHI KATI YA BIASHARA MARA NA AZAM FC BURE.
MASHABIKI 50 WAKWANZA KUCHANJA KUSHUHUDIA MECHI KATI YA BIASHARA MARA NA AZAM FC BURE.
Na WAF - Mwanza
Kuelekea mchezo unao tarajiwa kuchezwa siku ya jumanne ya terehe 22 februari 2022 kati ya Biashara mara na Azam fc mashabiki wa mpira na wananchi wa mkoa wa Mwanza kwa ujumla washauriwa kupata chanjo dhidi ya Uviko -19 na wananchi 50 wakwanza watakao chanja kupata fursa ya kushuhudia mechi hiyo bila kiingilio,
Yamesemwa hayo leo katika uwanja wa CCM kirumba na katibu msaidizi - chama cha soka mkoa wa Mwanza Bw. Khalid Bitebo akiongea na vyombo vya habari juu ya mchezo huo utakao chezwa kesho uwanjani hapo,
Bw Khalid Bitebo amesema wananchi na mashabiki wa mpira wa miguu wajitokeze kwa wingi kupata chanjo dhidi ya Uviko - 19 ili kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya ugonjwa huo,
"Tunapenda kuwapa taarifa kwamba Kesho kutakuwa na zoezi la kuchanja chanjo ya Uviko - 19 katika uwanja wa CCM kirumba na wananchi 50 wakwanza watakao chanja watapata fursa ya kuingia uwanjani bure bila malipo " Amesema Bw. Khalid Bitebo,
Aidha kocha wa timu ya Biashara Mara Bw. Vivier Bahati amewaasa mashabiki wa mpira wa miguu kuhamasika kupata chanjo dhidi ya Uviko -19 ili kuimarisha afya zao,
"Mimi binafsi nimechanja mapema sana na nina imani kila mtu anatamani afya yake iwe vizuri, niwaombe kila mtu ahamasike kupata chanjo ya Uviko - 19, itakuwa vizuri hata uwanjani utamgusa mwenzako bila shida na kupata matokeo mazuri " amesema Bw. Vivier Bahati,
MWISHO.
Comments
Post a Comment