𝐇𝐀𝐊𝐔𝐍𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐔𝐙𝐔𝐈𝐀 𝐑𝐎𝐁𝐎 𝐅𝐀𝐈𝐍𝐀𝐋𝐈 𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐒𝐇𝐎 - 𝐓𝐑𝐘 𝐀𝐆𝐀𝐈𝐍

 𝐇𝐀𝐊𝐔𝐍𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐔𝐙𝐔𝐈𝐀 𝐑𝐎𝐁𝐎 𝐅𝐀𝐈𝐍𝐀𝐋𝐈 𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐒𝐇𝐎 - 𝐓𝐑𝐘 𝐀𝐆𝐀𝐈𝐍


➪Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah Muhene 'Try Again' amesema kwa mikakati waliyojiwekea, basi ngumu kutokea timu ya kuwazuia kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.


➪Simba wameipata jeuri hiyo baada ya kukaa kileleni katika Kundi D wakikusanya pointi nne mbele ya ASEC Mimosas, RS Berkane na US Gendarmerie.


➪Akizungumza baada ya Simba kupata sare ya 1-1 ugenini dhidi ya US Gendarmarie, Try Again alisema usiri mkubwa uliokuwepo kambini baada ya baadhi ya wachezaji kuugua ghafla, ulichangia kwa kiasi kikubwa wao kupata matokeo mazuri ugenini


➪Try Again alisema kabla ya mchezo huo, wachezaji wao akiwemo Jonas Mkude, aliugua ghafla, lakini hakuna mtu kutoka nje ya kambi hiyo ambaye alifahamu na kuwafanya wapinzani wakutane na sapraizi uwanjani


➪"Haikuwa kazi rahisi kupata matokeo haya hapa ugenini, vijana wetu walipambana sana kutokana na kucheza katika mazingira magumu"


➪"Moja ya ugumu tuliokutana nao ni hali ya hewa ambayo ilikuwa nzito iliyosababisha baadhi ya wachezaji wetu kuugua ghafla mara baada ya kutua hapa nchini"


➪"Pia mazingira ya hoteli zilizopo hapa nyingi za ovyo ikiwemo hii tuliyofikia, kwa mfano leo (juzi) siku nzima hakukuwa na maji hotelini, siyo hujuma, lakini hali ya kiuchumi hapa nchini ndiyo imesababisha haya yote, lakini tunashukuru hatujapoteza mechi"


➪"Hivi sasa nguvu na akili zetu tunazielekeza katika mchezo unaofuata dhidi ya Berkane, tayari tumeanza maandalizi hayo," alisema Try Again


➪Simba wanatarajiwa kuwasili Morocco leo kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya RS Berkane ambao utapigwa Jumapili, Februari 27


➪Simba itaweka kambi ya siku nne katika jiji la Casablanca kabla ya kuelekea Berkane


Comments

Popular posts from this blog

Shafii Dauda Nipo Huru Sijafungiwa Na TFF

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes