Kutoa Mimba Sasa Ruksa
Colombia imekuwa Nchi ya 4 kutokea Amerika Kusini kuhalalisha utoaji mimba kwa Wanawake, hii ni baada ya Mahakama ya Kikatiba ya taifa hilo kupiga kura ya kuhalalisha utoaji wa mimba hadi wiki ya 24 ya ujauzito.
Sio Watu wote walioikubali sheria hii na sio wote walioipinga, wengi wa waliokubaliana nayo wanasema itasaidia Wanawake laki nne kila mwaka kuachana na mimba ambazo wamezipata kinyemela ikiwemo kwenye vitendo vya kubakwa.
Kabla ya uamuzi huu, Colombia ilikua inaruhusu utoaji mimba wakati tu maisha ya Mwanamke yapo hatarini au kama ujauzito uliotokana na ubakaji lakini sasa kwenye sheria hii mpya Wanawake wa Colombia wataweza kutoa mimba hadi wiki ya 24 ya ujauzito wao bila kutoa sababu zozote na itakua ni uamuzi wao.
Nchi nyingine za Amerika ya Kusini ambazo jambo hili limehalalishwa ni Argentina, Uruguay na Cuba ambazo huruhusu utoaji wa mimba bila vikwazo hadi hatua fulani za ujauzito.
Comments
Post a Comment