Posts

Showing posts from March, 2022

Wachezaji wa Simba sc wanaomaliza mikataba yao msimu huu ;

Image
 - Beki wa klabu ya Simba sc Joash Onyango (28) 🇰🇪 amekataa ofa mpya aliyopewa na klabu ya Simba kwa ajili ya kuongeza mkataba mpya katika klabu hiyo. - Beki huyo anataka aongezewe dau ili asaini mkataba mpya kwa wekundu wa Msimbazi ... Wakati huohuo klabu ya Orlando Pirates 🇿🇦 imeonesha nia ya kutaka saini yake. . . Wachezaji wa Simba sc wanaomaliza mikataba yao msimu huu ; 🇹🇿 Aishi Manula. 🇰🇪 Joash Onyango. 🇷🇼 Meddie Kagere. 🇨🇩 Chriss Mugalu. 🇹🇿 Mzamiru Yassin. 🇬🇭 Bernard Morrison. 🇹🇿 Erasto Nyoni. 🇹🇿 Ibrahim Ame 🇹🇿 Said Ndemla. 🇨🇮 Pascal Wawa. 🇹🇿 Hassan Dilunga.

Steve Nyerere Nikitenguliwa Nakwenda Mahakamani

Image
 "Sijiuzulu Wa Wala Sitoki, Nina Nia Ya Kuendeleza Industry Ya Mziki Nchi Hii.” Amesema Msemaji Wa Shirikisho La Muziki Tanzania (SMT) Steven Mengere, Maarufu Steve Nyerere Na Kuongeza Kwamba Uteuzi Wake Ukitenguliwa Atakwenda Mahakamani. 

KOMBE LA SHIRIKISHO CAF SIMBA SC WAHAHA

Image
Leo Jumapili, Machi 20, 2022 . ASEC MIMOSAS vs SIMBA SC ⏰ 19:00 🏟️ Stade de l'Amitié Cotonou Benin Kinara wa kundi D Simba SC (pointi 7) atashuka katika dimba la Stade de l'Amitie kuchuana na wenyeji Asec Mimosas (alama 6) katika marudiano ya hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho. Huu ni mpambano muhimu ambao utaamua hatma ya kundi hili. . Baada kushinda 3-1 katika dimba la Benjamin Mkapa na kuvunja mwiko wa Asec Mimosas wa kutokufungwa, Simba SC itahitajika kuvunja mwiko mwingine wa Asec Mimosas wa kutokupoteza nyumbani. . WACHEZAJI WA KUCHUNGWA: . ASEC MIMOSAS Kwa upande wa Asec Mimosas, chipukizi Karim Konate amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu akiwa amefumania nyavu mara 9 katika mechi 10 mpaka sasa. . SIMBA SC 🇹🇿 Mshindi mara mbili wa tuzo ya goli bora la wiki la #CAFCC Pape Sakho atakuwa alama ya kiulizo kwa kamati ya ulinzi ya Asec Mimosas. . Simba SC itawahitaji wachezaji wake wote kuwa katika ubora wao ikiwa inahitaji ushindi ili kukata tiketi ya robo fainali. ....

Yanga Sc Vs Kmc Mambo Ni Mengi Mda Ni Mchache

Image
 - Kuelekea mchezo wa kesho Yanga dhidi ya KMC kutakuwa na surprise nyingi kabla ya mchezo utakaochezwa saa 1 usiku. - Klabu ya Yanga imeidedicate mechi hiyo kwa Rais Samia Suluhu ambaye ametimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani. - Utachezwa mchezo wa utangulizi baina ya Viongozi wa Yanga na GSM wakiongozwa na Haji Manara dhidi ya timu ya Bongo fleva. - Utachezwa mchezo mwingine wa utangulizi, Yanga princess v Ilala queens. - Huenda Rais Samia Suluhu akahudhuria mchezo huo, pia kutakuwa na burudani zingine za wasanii.

Robo Fainali Ya Uefa Itakuwa Hivi

Image
 🚨Robo Fainali Ya Uefa Itakuwa Hivi  ✍️Chelsea Vs Real Madrid  ✍️Mancity vs Atletco Madrid  ✍️Benfica vs Liverpool  ✍️Villa Real vs Bayern Munich  ✍️Mshindi baina ya Man city na Atletco atacheza na mshindi baina ya Chelsea na Madrid kunako nusu Fainali . ✍️Mshindi Baina ya Benfica na Liverpool atacheza na mshindi baina ya Villareal na Bayern Nusu fainali . Robo fainali itaanza tar 05 na 06 Aprili 2022 .#NYAKAHIYO. UBINGWA MSIMU HUU UNAUONA WAP?

CAF: SIMBA INAONGOZA KUTAZAMWA AFRIKA .

Image
Kwa mujibu wa CAF, Simba imekuwa ndio klabu inayotazamwa kwa wingi na mashabiki kupitia akaunti za mitandao ya kijamii za CAF, ikiwamo Youtube (CAF TV) kulinganisha na timu nyingine kongwe Afrika na ikifuatiwa na Al Ahly ya Misri. . Rekodi zinaonyesha pambano lililotazamwa zaidi ni lile la Simba vs Al Ahly la msimu uliopita ambapo Simba ilishinda 1-0, kwani lilitazamwa na mashabiki zaidi ya milioni moja, huku maoni yakiwa zaidi ya 800. . Mechi iliyoshika nafasi ya pili ni Simba na AS Vita iliyopigwa Dar ikitazamwa na mashabiki 597,000 na ile ya ugenini ambayo Simba ilishinda bao 1-0 ina watazamaji 529,000 katika chaneli ya CAF TV.

Romyjons Watanzania Nisameheni Nimekosa Mimi Nimekosa Mimi

Image
 @romyjons Ameomba Radhi Kwa Ndugu Jamaa Na Marafiki Kwa Yale Yote Yanayoendelea Katika Mitandao Ya Kijamii Ambayo Yanamuhusu Yeye Moja Kwa Moja. Kwenye Insta Story Yake Ameandika..........""Naomba Radhi Kwa Ndugu, Jamaa Na Marafiki Zangu Pamoja Na Mke Wangu Na Watanzania Wote Kwa Ujumla ...Kwa Yote Yanayoendelea Mitandaoni....Yallah Atusamehe Madhambi Yetu Ya Kusudi Na Yasiyo Kusudi...Na Atujaalie Mwisho Mwema Inshalaah"

Simba Sc Yaingia Mawindoni Wachezaji Wanne Watupiwa Vilango

Image
 “Mpango wetu katika dirisha lijalo, tutasajili wachezaji wanne wa daraja la juu wa kimataifa ambao ni mastraika wawili, winga mmoja na beki wa kati mmoja. Ni wachezaji hasa na watakuwa na mchango mkubwa kwa timu,”  - Salim Abdallah "Try Again", Mwenyekiti wa Bodi ya klabu ya Simba SC.

TANGAZA NASI BIASHARA YAKO KWA BEI NAFUU ZAIDI

Image
 TANGAZA NASI BIASHARA YAKO KWA BEI NAFUU ZAIDI      KUTANGAZA , KUNUNUA , KUUZA BIDHAA ZAKO      WASILIANA NAMI KWA NAMBA +255 769 230 966  Kwa mauzo au manunuzi na kuuza bidhaa yako wasiliana  Nami kwa namba +255769230966 au njoo Whatsapp Kwa  Namba hiyo hiyo

Ng'ombe Wa Fiston Mayele Atua Jangwani

Image
Ng'ombe aliyepewa mshambuliaji wa @yangasc Fiston Mayele baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao Yanga ilishinda 2-0 kwenye uwanja wa Manungu Morogoro amefikishwa makao makuu ya klabu Jangwani Dar es Salaam.

Kocha wa RS Berkane Simba Sc Wamestahili Ushindi

Image
 Kocha wa RS Berkane 🇲🇦 "Samahani na mambo mengi ya kuongea kama mtaniruhusu nitumie kifaransa. Ok kama haiwezekani ntatumia kingereza hivyohivyo" "Nawapongeza Simba kwa ushindi, wamestahili, wamepata point ugenini pia nchini Niger. Tunatakiwa kusahau kilichotokea na kujiandaa na mchezo ujao, mechi imeisha tunapaswa kuwa fair" "Nimeshindwa kupata points mara mbili katika uwanja wa Benjamin Mkapa sababu Simba ni timu bora" "Kocha wa Simba amesema Berkane si chochote si lolote (CAF) wanapaswa waitoe kwenye Mashindano,, Kauli kama hizo ni aibu kutolewa na kocha mkubwa kama yeye, tunamtakia kila lakheri kwenye michezo yake inayofuata"

Kocha wa Simba sc aishauri (CAF) iiondoe kwenye Mashindano klabu ya RS Berkane 🇲🇦.

Image
Waamuzi nao ni binadamu wanaweza kufanya makosa. Siwezi kusema ile ilikuwa Offside au sio offside, kama haikuwa Offside basi tulifanya makosa lakini tulikuwa na bahati" "Vitendo vya vurugu walivyovifanya RS Berkane 🇲🇦 nawashauri (CAF) hii timu waiondoe kwenye Mashindano kwa sababu wameshindwa kuheshimu taratibu za mpira" "Tulikuwa bora zaidi yao, tulimiliki mchezo na kutengeneza nafasi nyingi ambazo tungezitumia vizuri tungepata ushindi mnono zaidi. Tulihakikisha hatuwapi nafasi ambazo zingetuletea madhara" "Tuliamua kutumia udhaifu wao hasa upande wa kushoto, tuliweka Wachezaji ambao wanaweza kuzuia mipira yao ya kutenga na tulifanikiwa muda mwingi wa mchezo

Rs Berkane Watua CAF Refa Ameongwa Pesa Na Simba Sc

Image
 RASMI : Klabu ya RS Berkane ya Morocco imewasilisha malalamiko kwa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuhusu mwamuzi wa DR Congo, Jacques Ndala Chuma alichezesha mchezo dhidi ya Simba SC na kutaka afungiwe. Berkane wanadai Ndala alihongwa ndio maana aliwanyima penati kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Pia wanasema walipata bao la wazi lakini walinyima kwa sababu kwa sababu mchezaji wao alikuwa tayari ameshaotea (offside). Wamorocco hao walisema, Simba ilipoteza muda mwingi na mwamuzi wa akiba akaongeza dakika nne tu za kuchezwa. Klabu hiyo inaitaka CAF kumuadhibu mwamuzi na wasaidizi wake wote kwa kufungiwa ikiwezekana kwa kushindwa kutenda haki katika mchezo huo uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Yanga Sc Kucheza Mchezo Wa Kimataifa Na Somalia

Image
 - Klabu ya Yanga sc itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa Jumamosi hii March 12, 2022 na timu ya taifa ya Somalia 🇸🇴 saa 1 isiku Azam complex. - Lengo la mchezo huo ni kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia taasisi ya ALI KIMARA / Ali Kimara Rare disease foundation. "Sisi kama klabu ya Yanga kwa kushirikiana na GSM foundation tutachangia taasisi ya Ali Kimara na kuwaelimisha Watanzania wapate uelewa mpana juu ya maradhi haya adimu" 🔍 Haji Manara msemaji wa Yanga.

𝙍𝙤𝙢𝙖𝙣 𝘼𝙗𝙧𝙖𝙢𝙤𝙫𝙞𝙘𝙝 𝙖𝙬𝙚𝙠𝙚𝙬𝙖 𝙫𝙞𝙠𝙬𝙖𝙯𝙤

Image
 Mali zote za Roman Abramovich zipo chini ya Serikali ya Uingereza kuanzia sasa..  Kulingana na vikwazo vipya, Chelsea itaendeshwa chini ya leseni maalum huku mfumo wa mishahara ukiwa unafuatiliwa.  •Mali zote za Roman Abramovich (Uingereza) zipo chini ya Serikali ya Uingereza •Chelsea bado wanaweza kufanya kazi chini ya leseni maalum lakini mauzo ya jezi yamesitishwa. •Hakuna uhamisho wa wachezaji wapya au mikataba mipya inayoruhusiwa •Hakuna mauzo ya bidhaa yanayoruhusiwa, duka la klabu limefungwa. •Klabu haitaruhusiwa kuuza tiketi mpya labda wale walio nunua tiketi za msimu mzima ndio wanaweza kwenda uwanjani  •Hakutakuwa na mashabiki wa ugenini siku zijazo. • Abramovich amezuiwa kuiuza Chelsea FC na mali yake yote nchini ya Serikali ya Uingereza  •Iwapo Chelsea itauzwa, fedha hazitakwenda kwa namna yoyote kwa Abramovich

VILABU 10 BORA KWA MUJIBU WA #IFFHS- Africa. (World)

Image
 VILABU 10 BORA KWA MUJIBU WA  #IFFHS- Africa. (World) 1. 🇪🇬 Al Ahly - (20) 2. 🇪🇬 Pyramids - (55) 3. 🇲🇦 Wydad - (78) 4. 🇿🇦 Sundowns - (92) 5. 🇹🇿 Simba - (98) 6. 🇩🇿 CR Belouizdad - (104) 7. 🇩🇿 JS Kabylie - (113) 8. 🇦🇴 Petro Luanda - (133) 9. 🇹🇳 CS Sfaxien - (136) 10. 🇹🇳 ES Tunis - (141)

Putin Marekani Yumo Na Uingereza

Image
 Serikali ya Urusi leo imeidhinisha na kutaja majina ya Nchi ambazo zimeonesha vitendo visivyo vya kirafiki kwa Urusi baada ya kuivamia Kijeshi ikiwemo kuiwekea vikwazo na Kampuni zake kuondoka Urusi, Serikali ya Urusi imesema inatafakari hatua ambazo itachukua kwa Nchi hizo. Nchi zilizotajwa ni Marekani, Canada, Australia, Iceland, Japan, Monaco, Montenegro, New Zealand, Norway, Taiwan, San Marino, Singapore, Korea Kusini, Switzerland , Ukraine na Mataifa yote ya Umoja wa Ulaya ikiwemo Uingereza.

MCHEZO WA SIMBA SCUMEREJESHWA SAA MOJA

Image
Ahmed Ally :-Mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji Fc umerejeshwa katika muda wake wa awali wa saa 1:00 Usiku, badala ya saa 10:00 Jioni iliyotangazwa leo siku ni Ile ile Jumatatu 🔥🔥💪🏻

𝐊𝐈𝐊𝐎𝐒𝐈 𝐂𝐇𝐀 𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐒𝐂 𝐃𝐇𝐈𝐃𝐈 𝗬𝗔 𝗚𝗘𝗜𝗧𝗔 𝗚𝗢𝗟𝗗 𝗙𝗖

Image
 𝐊𝐈𝐊𝐎𝐒𝐈 𝐂𝐇𝐀 𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐒𝐂 𝐃𝐇𝐈𝐃𝐈 𝗬𝗔 𝗚𝗘𝗜𝗧𝗔 𝗚𝗢𝗟𝗗 𝗙𝗖 1: Djigui Diarra 2: Paul Godfrey 3: Yassin Msatafa 4: Bakari Nondo ©️ 5: Dickson Job 6: Yannick Bangala 7: Denis Nkane 8: Salum Abubakari "Sure boy" 9: Fiston Mayele 10: Feisal salum 11: Deus Kaseke 𝙎𝙐𝘽 Mshery, Balama, Makambo, Ambundo, , Mauya, Yusufu, Kibwana, Mauya,  Bacca.

Mwinyi Zahera :Fiston Mayele Ana Kila Sababu Kuwa Mfungaji Bora

Image
 Kocha wa zamani wa Klabu ya Yanga SC ambaye kwa sasa ndiye Mkurugenzi wa Soka la Vijana wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema Fiston Mayele 🇨🇩 ana kila sababu ya kuwa Mfungaji Bora msimu huu labda tu azembee mwenyewe. Zahera amesema msimu huu Yanga wameimarika kuanzia eneo la Golikipa mpaka mshambuliaji wa mwisho Kiasi kwamba uhakika wa yeye kufunga Magoli na kuibuka Mfungaji Bora wa NBC Premier League inawezekana. “Yanga ina wapishi wengi wa mabao na Mayele naona kabisa ana kila sababu ya kuchukua tuzo hiyo na hata mwenyewe niliwahi kumueleza hivyo,” “Mayele amekuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza anacheza zaidi ya dakika 80, kila mechi tena kwenye timu iliyoimairika kuanzia kipa hadi mbele, kazi ni kwake mwenyewe ila hakuna sababu ya kumzuia na kushindwa kufanya hivyo.”

Shabiki Gormahia Aibuka Na Jiwe Uwanjani

Image
 Baada ya wiki hii kusambaa kwa picha ya Shabiki wa Gor Mahia Winnie Nyar Kasagam zikimuonyesha akiwa na jiwe kubwa kwaajili ya kumpiga moja ya askari wa uwanja wa Kasarani 🇰🇪 hatimaye dada huyo amefunguka mkasa mzima ulivyokuwa "Unajua Mimi ni mtu mtulivu sana, Winnie uliyemwona akibeba jiwe uwanjani hakuwa Winnie ambaye kila mtu anamjua,"  "Siku hiyo, nilichanganyikiwa kihisia, moyo wangu ulikuwa unauma. Na unajua, wakati wa maumivu ya moyo, akili na mwili hujibu. "Mpenzi wangu alikuwa amevamiwa, Ilinikasirisha sana kwa sababu ananisaidia kifedha, na ndiye tegemeo katika uhusiano wetu. "Mwanzoni, kulikuwa na tetesi kuwa ameuawa, hivyo nikatoka nyumbani hadi uwanjani kumuangalia mpenzi wangu Odinga, Nilipoingia uwanjani nikamkuta amelala chini amepoteza fahamu. . "Hilo liliamsha hasira kali ndani yangu, mara moja, nilichukua jiwe kwenda kumtafuta mtu ambaye alimvamia mpenzi wangu"  "Nilipofika alipo, nilishtuka baada ya kugundua ni mtu ambaye ...

YANGA YAKOMBA TUZO ZOTE.

Image
Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Yanga SC Said Ntibazonkiza 🇧🇮 ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu ya NBC 🇹🇿 Pia Kocha Mkuu wa Klabu hiyo,Nasreddine Nabi 🇹🇳ametwaa tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi February.

Simba Sc Shomari Kapombe Pumzika Kwanza

Image
 Beki wa Klabu ya Simba SC,Shomary Kapombe ataukosa Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Kati ya Simba SC dhidi ya Dodoma Jiji baada ya kupewa mapumnziko ya siku tano na Madaktari wa Simba SC licha ya kuwa yupo fiti.  Kapombe hapo Juzi aliruhusiwa kutoka hospitali alipopelekwa usiku baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu (NBC Premier League) dhidi ya Biashara. Baada ya vipimo Kapombe alibainika kuwa hajapata madhara yoyote ya kichwa yuko salama tofaut na ilivyotarajiwa

MABADILIKO YA MUDA WA MCHEZO SIMBA SC VS DODOMA JIJI

Image
 MABADILIKO YA MUDA WA MCHEZO. . Mechi yetu ya kesho ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji ambayo awali ilikuwa ichezwe saa moja usiku, sasa itapigwa saa 10 jioni. Tayari uongozi wa klabu umepokea taarifa ya maandishi kutoka Bodi ya Ligi kuhusu mabadiliko hayo ya muda wa mchezo. Maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri kila kitu kipo kama kilivyopangwa na kinachosubiriwa ni muda tu ufike mchezo huo upigwe tuendelee ku enjoy.

Wydad Casablanca Yampeleka FIFA Simon Msuva

Image
 Wydad Casablanca ya Morocco, wamemshtaki Mchezaji Mtanzania Simon Msuva kwa Shirikisho la soka Duniani (FIFA) kuwa amevunja mkataba bila sababu. Hata hivyo, Msuva naye amewashtaki Wydad kwa FIFA pia kuwa hajalipwa pesa zake muda mrefu na miamba hiyo ya Afrika. Kesi hizo zimemuweka njia panda Msuva ambaye alikuwa anakaribia kumalizana na timu moja huko Uturuki ambapo sasa atasubiri kesi hizo FIFA zimalizike kujua hatma yake. Msuva bado amesalia nchini akigoma kuendelea kuichezea klabu hiyo kutokana na kutomlipa fedha zake kwa muda mrefu

PAPE OSMANE SAKHO: Kapombe Ni Rafiki Yangu

Image
 “Kapombe yuko na sifa nyingi kulingana na mahitaji ya beki wa kulia, ndio maana amekuwa akinivutia mpaka amekuwa rafiki yangu wa karibu hata tukiwa nje ya maisha ya timu.”  “Nashukuru kwa wakati huu nimekuwa kwenye kiwango ingawa sio katika ubora kama ule ambao naamini ninao bado nahitajika kujitoa zaidi na kusaidia timu.” PAPE OSMANE SAKHO.

Luis Miquisson Simba Sc Kutwaa Ubingwa Ligi Kuu Bara

Image
 Winga wa zamani wa Simba, Luis Miquissone 🇲🇿 anasema kutokana na mwenendo wa Ligi Kuu Bara ulivyo msimu huu bado timu ya Simba inaweza kutwaa ubingwa na ikautetea kwa mara ya tano mfululizo. "Bado naipa nafasi kubwa timu yangu (Simba) kufanya hivyo lakini hata katika mashindano mengine kama kombe la Shirikisho (ASFC), nalo wanaweza kufanya vizuri na kuchukua ubingwa” SOURCE : GOAL AFRICA.

ROBERTO CARLOS AFUNGA GOLI LAKE LA KWANZA BULL IN THE BARNE FC:

Image
 ROBERTO CARLOS AFUNGA GOLI LAKE LA KWANZA BULL IN THE BARNE FC: Nguli wa Brazil na mshindi wa kombe la Dunia Roberto Carlos alicheza mechi yake ya kwanza klabu yake mpya ya Bull In The Barne FC inayoshiriki Ligi ya ya Jumapili ya wilaya huko England. Katika mchezo uliochezwa siku ya Ijumaa Bull In The Barne ilifungwa 4-3 na Harlescott  katika mchezo wa kirafiki ambapo Carlos alifunga moja ya magoli kwa mkwaju wa penalti.

HAKUTAKUWA NA KOMBE LA DUNIA MWAKA HUU".

Image
 "HAKUTAKUWA NA KOMBE LA DUNIA MWAKA HUU"...Putin Aionya FIFA kuingilia Mambo ya Kijeshi.. "Msithubutu kuingilia Mambo ya Kijeshi, Bakini kwenye Mpira wa Miguu",...Mkijaribu mjue hakutakuwa na Kombe la Dunia Qatar 🇶🇦. Putin amesema hayo jana akijibu swali la Mwandishi wa habari juu ya Adhabu kutoka FIFA.. "Huyo Mjinga Nani anayesema Russia haitashiriki Kombe la Dunia Qatar 2022?, nasema Russia Lazima Itacheza Kombe la Dunia mwaka huu, Aidha wapende ama wasipende..Sahau kuhusu Mzaha huo.. "Lazima nawaambia Lazima, Wakijaribu kutuzuia Basi wajue Mwaka huu hakutakuwa na Michezo hiyo". "Sipendi Double Standards za kipuuzi, hayajaanza Leo Mambo haya ya kivita, tumeshuhudia mara nyingi Mataifa ya Magharibi yakivamia na kupigana vita, Vietnam, Korea, Libya, Iraq, Syria, Amerika kusini, kati....na hata sisi akiwemo Ukraine tulipigana vita ndefu Afghanistan 🇦🇫, Sijawahi kuwaona Wala Kusikia FIFA akitenda haya... Mwamba Anakwambia wachague, Urusi irudi...

SIMBA SC KUWAKOSA NYOTA SITA DHIDI YA BIASHIARA;

Image
Katika mchezo wa leo Simba Sc itawakosa wachezaji sita kutokana na kuwa  majeruhi. Nyota hao ni: ▪️Aishi Manula  ▪️Chris Mugalu  ▪️Kibu Denis ▪️Hassan Dilunga ▪️Jonas Mkude ▪️Sadio Kanoute. NOTE:MUGALU na KIBU ambao walikuwa nje ya uwanja kwa muda, tayari wameanza mazoezi, na utimamu wao wa mwili ukiwa sawa wataanza kushuka dimbani.

Try Again tumezidiwa pointi 11, lakini tuna mechi 15 mbeleni

Image
 LICHA ya Yanga kutambia pointi 11 zaidi ilizoipiku Simba katika harakati za ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ ameonya wana mechi 15 watakazocheza kimkakati na wanaamini kushangaza wengi. Amesisitiza  “Sawa tunaanza mzunguko wa pili tukiwa tumezidiwa pointi 11, lakini tuna mechi 15 mbeleni, hivyo tusubiri, msiwe na haraka na mambo” Yanga Jumapili iliyopita ilifikisha pointi 42 na kujiimarisha kileleni kwenye msimamo ikiwapiku watani zao Simba kwa pointi 11 na kesho Wekundu wa Msimbazi wataikaribisha Biashara United ikiwa ni mechi yao ya kwanza ya mzunguko wa pili. Hadi sasa Simba ni ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 31 na ikishinda itafikisha 34 na kupunguza gepu la pointi Tofauti ya pointi hizo zimesababisha baadhi ya wapenzi wa Yanga kutamba  kasi hiyo haitoshuka kwenye mzunguko wa pili na kila timu ishinde mechi zake. Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema “Pointi 1...

Nimejitoa Kwenye "Ndondo" Cup Shafiih Dauda

Image
 Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa Soka nchini, Shaffih Daudi amesema kwamba amejitoa kwenye utaratibu wa kuandaa mashindano ya mpira wa miguu maarufuku kama 'Ndondo Cup' kwa sababu anatumikia adhabu ya TFF "Nimetii mamlaka (TFF). Mnafahamu kuwa nimefungia kujishughulisha na michezo”. Dauda alifungiwa February 16, 2022 kujihusisha na shughuli za Soka kwa kipindi cha Miaka 5 na kupigwa faini ya kiasi cha Million 6, kwa kosa la kuchapisha taarifa hisio na maadili kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes

Image
 #Repost @issamasoud with @make_repost ・・・ Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes] Tajiri na mmiliki wa Chelsea FC Roman Abramovich alijiwekea Kinga ya mkopo kwa Chelsea FC yenye thamani ya $2 billion. Na mwaka uliopita aliongeza tena mkopo wa $26 milion. Ikumbukwe Abramovich aliinunua Chelsea kwa $190 million mwaka 2003. Kwa mujibu wa Forbes] mpaka mwaka 2021 unaisha Chelsea FC ilikuwa na thamani ya $3.2 billion. Hivyo basi ikatokea Serikali ya Uingereza inazuia mali zake kutokana na kuwekewa vikwazo kwa sababu ya vita kati ya Ukraine vs Russia, Abramovich itabidi alipwe cash $2 bilioni ili aweze kuachia Club ya Chelsea umiliki wake. Na kama akiamua kuweka sokoni Club hiyo inahitajika mnunuzi atakaekuja kununua hiyo Club alipe market value kwa maana ya $3.2 billion hii ikiwa ni pamoja na deni la Abramovich la $2 bilion. Vinginevyo Club itaingizwa kwenye ufilisi sababu haina uwezo wa kulipa hiyo fedha Cash.

Korea Kaskazini Nasimama Na Urusi

Image
 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepiga kura kwa wingi ya kuunga mkono azimio la kuitaka Urusi kusimamisha mara moja mashambulizi nchini Ukraine na kuyaondoa majeshi yake yote, Mataifa 141 yameunga mkono azimio hilo dhidi ya matano ambayo yamepinga, kura hiyo iliyoitwa uvamizi dhidi ya Ukraine ilipigwa katika kikao cha dharura cha UNGA.  Urusi imeungwa mkono na Belarus, Syria, Korea Kaskazini na Eritrea, dalili inayoashiria namna Taifa hilo lilivyotengwa kimataifa.  Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Gutteres amesema  ujumbe wa UNGA uko wazi na Urusi inatakiwa kusimamisha mashambulizi hayo na kufungua milango ya mazungumzo na diplomasia. Kwenye kura hizo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uganda zipo kwenye orodha ya Nchi 34 ambazo zimejizuia kupiga kura kwenye upande wowote, huku Kenya ikiunga mkono Ukraine na kutaka Urusi iondoke Ukraine.

TUNAZITAKA POINTI TATU DHIDI YA SIMBA .

Image
Kocha Mkuu wa Biashara United, Vivier Bahati amefunguka kuelekea mchezo dhidi ya Simba SC: . “Hii mechi itakuwa ngumu sana kwa sababu tunacheza na Simba ambayo imetoka kupoteza mchezo wao wa kimataifa na wanapambana kutafuta pointi muhimu ili kujiweka katika nafasi ya kutetea ubingwa,” amesema Vivier na kuongeza; . "Tunahitaji kuanza vizuri mzunguko wa pili kwa kutafuta pointi dhidi ya Simba kama ilivyokuwa katika mchezo wa duru la kwanza.”

NYAKATI NGUMU KATIKA HISTORIA ZA SOKA

Image
 NYAKATI NGUMU  KATIKA HISTORIA ZA SOKA ▪️ Fabrice Muamba alipopata mshtuko wa moyo uwanjani wakati wa mechi kati Bolton Wanderers dhidi ya Tottenham Hotspours. ▪️Christian Eriksen alipopata mshtuko wa moyo akiwa katika majukumu yake ya kitaifa. ▪️Timu ya taifa ya Brazil kufungwa mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani kwenye kombe la dunia. ▪️Mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha alipofariki baada ya kuanguka na helkopta King Power Stadium. ▪️Ajali ya ndege waliyopata wachezaji na viongozi wa timu ya Chapecoence na kuua watu 71 kati ya 77 waliokua kwenye ndege hiyo. ▪️2010 kombe la dunia Luis Suarez anashika mpira uliokua unaelekea golini na Ghana anashindwa kutinga nusu fainali. ▪️2006 Zidane anapewa kadi nyekundu kwa kupiga kichwa Materazzi na kukosa kombe la dunia. ▪️Messi alipotangaza kuondoka rasmi Barcelona na kwenda kujiunga na Paris Saint Germany. ▪️Aguero kutangaza kustaafu soka baada ya kupata matatizo ya moyo. ▪️Ronaldo De Lima alipotangaza kustaafu soka. ▪️Andre...

Wallace Karia Wachambuzi Wanaua Mpira

Image
 Rais wa shirikisho la soka Tanzania ! "Kuna wanaojiita wachambuzi, sijui uchambuzi wamesomea wapi. Kusema ukweli katika watu ambao hawautendei haki mpira wetu ni WACHAMBUZI" "Mimi ninaona wao (Wachambuzi) ndio wakati mwingine wanaopotosha na kuleta taharuki" 🔍 Wallace Karia

Nimeamua Kuiza Chelsea Roman Abromavich

Image
 Bilionea ambaye ni Mmiliki wa Club ya Chelsea ya England Roman Abramovich amethibitisha kuwa anataka kuiuza club hiyo ambapo anafanya hivi kwa maslahi mapana ya Club, Wadhamini na Wafanyakazi wa Club. “Ningependa kutoa taarifa kuhusiana na tetesi zinazoendelea kwenye vyombo vya habari kuhusiana na umiliki wangu Chelsea, siku zote nimekuwa nikifanya maamuzi kwa sababu ya maslahi ya club, kwa hali inavyoendelea sasa nimeamua kuiuza club” ——— Roman Abromavich. Roman aliinunua club hiyo 2003 kwa pound milioni 140 (Tsh Bilioni 433) na sasa ameamua kuiuza baada ya vita ya Ukraine kuisababishia Russia na Wawekezaji wake kuwekewa vikwazo au biashara zao kusitishwa sehemu mbalimbali. Kwa mujibu wa Forbes Chelsea sasa ina thamani ya pound Bilioni 2.4 (Tsh Trilioni 7.4). Roman katika taarifa iliyotolewa na Chelsea anasema atauza club hiyo na pesa zote alizouza zitaenda katika mfuko maalum wa kusaidia Waathirika wa vita nchini Ukraine na wala hana lengo la kujipatia Faida

Mario Balotelli:

Image
 Mario Balotelli: "Kama ningekuwa na akili yangu ya sasa nilipokuwa Manchester City pengine ningeshinda mpira mmoja wa dhahabu (Ballon D'or). Nina uhakika na hilo." "Nilipokua nilijua sikupaswa kuondoka Manchester City wakati huo. Miaka yote hii City imekuwa bora zaidi. Ningeweza kuwa hapa kama Sergio Aguero kwa muda mrefu."

Abramovich anataka kuiuza Chelsea haraka iwezekanavyo

Image
Bilionea wa Uswizi Hansjorg Wyss amethibitisha kuwa Abramovich anataka kuiuza Chelsea haraka iwezekanavyo: "Roman Abramovich anataka kujiondoa Chelsea haraka iwezekanavyo.. Mimi na watu wengine watatu tulipokea ofa Jumanne ya kuinunua Chelsea kutoka kwa Abramovich.. Anataka pesa nyingi kwa sasa.". "Hatujui bei halisi ya kuinunua. Ninaweza kufikiria vizuri sana kuingia na washirika. Lakini lazima nichunguze masharti ya jumla kwanza. Lakini ninachoweza kusema, hakika nisingeweza kufanya jambo kama hilo peke yangu." "Lazima nisubiri siku nne hadi tano sasa. Abramovich anataka pesa nyingi kwa sasa. Najua Chelsea inadaiwa karibu pauni bilioni 2. Lakini Chelsea haina pesa. Ina maana kwamba wale wanaokwenda kuinunua Chelsea wanapaswa kuchukua nafasi ya Abramovich."  

SHIRIKISHO LA SOKA LA URUSI YAILALAMIKIA FIFA NA UEFA.

Image
 SHIRIKISHO LA SOKA LA URUSI YAILALAMIKIA FIFA NA UEFA. "Shirikisho la soka la Urusi limesikitishwa na taarifa ya kutoka FIFA pamoja na UEFA ya kuwatoa kushiriki kombe la dunia na kusimamisha ushiriki wa timu ya taifa na vilabu kwenye mashindano  yanayoandaliwa na vyama hivyo vya soka duniani". "Chama cha soka Urusi kinaona hatua hizo zilizochukuliwa juu yao ni ya uonevu kwao". "mpira unahusisha jopo kubwa la wachezaji makocha,waamuzi na viongozi wa vilabu kutoka nchi tofauti na wakiwa na mikataba". "Pia tutakua tunawakosea mamilioni ya mashabiki waliokua Urusi pamoja na nje ya Urusi ambao wanafatilia timu za Urusi pamoja na wachezaji wa kwenye mataifa yao". Uongozi wa Sparkat Moscow ✍️ "Tumesikitishwa sana na taarifa kutoka UEFA ya kutolewa katika mashindano ya UROPA tuliyokua tunashiriki". "Wachezaji wetu walitumia nguvu kubwa,akili nyingi pamoja na umakini wa hali ya juu lakini ndiyo mambo ya soka hatuwezi kupingana nayo".

WANANCHI mmesikia mnadaiwa __!!

Image
 MTIBWA: YANGA HAWAJALIPA PESA YA MSHERI . "Yalifanyika makubaliano ya pande mbili tukiamini Yanga ni watu wazima na watatelekeza mkataba unavyosema, lakini mpaka sasa hakuna hata moja lililofanyika.  . “Tangu January mpaka sasa hatujaona kitu. Mbaya zaidi Mawasiliano yetu na wao sio mazuri na hatukutaka haya mambo yafike kwenye Vyombo vya Habari, lakini kinachofanyika sasa ni sisi kuwafuata wao, lakini ilitakiwa wao watufuate sisi.  . “Hii ni kama tunawambeleza juu ya malipo ya Abuutwalib Mshery. Tunaendelea kuwasubiri na tutakuwa wapole, lakini hawajafanya vile ambavyo tulitarajia. Mtibwa Sugar tumetoa vijana wengi kwenda Yanga,  kikubwa watazame makubaliano yetu na wao yanasemaje" - Thobias Kifaru (Msemaji wa Mtibwa Sugar) . WANANCHI mmesikia mnadaiwa __!!😂

Baba Mzazi wa Mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) amefariki dunia

Image
 Mzee Said Mohamed ambaye ni Baba Mzazi wa Mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) amefariki dunia alfajiri ya leo March 1 2022 na anatazikwa leo saa kumi jioni kwenye makaburi ya kisutu Dar es salaam. Marehemu Mzee Said ni Mfanyabiashara wa muda mrefu Tanzania ambapo alianzisha biashara ya kwanza mwaka 1955 kwa kuuza bidhaa ndogondogo Tanga lakini baadae alihamia kuuza nguo na kuhama kutoka Tanga hadi Songea ambako alijitanua katika kilimo cha korosho ambacho Familia yake imekiendeleza hadi leo. Marehemu Mzee Said alistaafu mwaka 1996 na kuruhusu kizazi kilichofuatia kuchukua usukani wa kila siku wa biashara na kuamua kuhamia Dar es Salaam na kuwa Wasambazaji wakubwa wa mazulia ya PVC ndani ya Tanzania na nchi jirani.  Inna lillahi wa inna ilayhi rajuun 🙏🏿

KAMA VIPI TUKUTANE kwa Mkapa, BERKANE YATIBUA MAMBO.

Image
 KAMA VIPI TUKUTANE kwa Mkapa, BERKANE YATIBUA MAMBO.   SIMBA ilipoteza mechi ya kwanza kwenye mechi za makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kunyukwa na RS Berkane kwa mabao 2-0, lakini ikajifariji kwa kusema itamaliza kazi Kwa Mkapa. Simba ilikumbana na kipigo kwenye Uwanja wa Berkane, Morocco katika mechi ya Kundi D iliyopigwa kuanzia saa 4:00 usiku na kuifanya ing’oke kileleni hadi nafasi ya pili ikisaliwa na pointi 4 sawa na ilizonazo USGN ya Niger iliyoitoa nishai ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa kuilaza 2-0 katika mechi ingine ya kundi hilo. Mabao mawili ya Adama Ba dakika ya 32 na Charki El Bahri dakika ya 41 yakitokana na makosa ya safu ya ulinzi ya Simba ilitibua rekodi ya Mnyama kundini. Kocha Pablo Franco aliwaanzisha Nahodha John Bocco na Kennedy Juma badala ya Meddie Kagere na Yusuph Mhilu walioanza katika kikosi kilichovaana na USGN na kutoka nao sare ya 1-1 wiki iliyopita. Berkane ilianza kwa kasi, japo kipindi cha pili Simba ilirudi kivingi...

NABI BADO SIJAFIKA UBORA NINAO UTAKA

Image
 BADO SIJAFIKA UBORA NINAO UTAKA  Kocha wa mabingwa wa kihistoria Tanzania, Nasaradine Mohamed Nabi amesema kuwa kikosi chake bado hakijafika level ya ubora anao utaka yeye licha ya siku 90 alizoomba kumalizika  Nabi amesema kuwa kwa sasa kikosi kimeimarika zaidi japo bado hajafika kwenye kiwango anacho kitaka hivyo kuna kazi kubwa inatakiwa kuendelea kufanyika katika uwanja wa mazoezi. Katika hatua nyingine wachezaji wa Yanga wanatarajia kuingia kambini Leo baada ya mapumziko ya siku moja  Yanga inajiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold utakao chezwa uwanja wa CCM KIRUMBA Mwanza.