Mwinyi Zahera :Fiston Mayele Ana Kila Sababu Kuwa Mfungaji Bora
Kocha wa zamani wa Klabu ya Yanga SC ambaye kwa sasa ndiye Mkurugenzi wa Soka la Vijana wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema Fiston Mayele 🇨🇩 ana kila sababu ya kuwa Mfungaji Bora msimu huu labda tu azembee mwenyewe.
Zahera amesema msimu huu Yanga wameimarika kuanzia eneo la Golikipa mpaka mshambuliaji wa mwisho Kiasi kwamba uhakika wa yeye kufunga Magoli na kuibuka Mfungaji Bora wa NBC Premier League inawezekana.
“Yanga ina wapishi wengi wa mabao na Mayele naona kabisa ana kila sababu ya kuchukua tuzo hiyo na hata mwenyewe niliwahi kumueleza hivyo,”
“Mayele amekuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza anacheza zaidi ya dakika 80, kila mechi tena kwenye timu iliyoimairika kuanzia kipa hadi mbele, kazi ni kwake mwenyewe ila hakuna sababu ya kumzuia na kushindwa kufanya hivyo.”
Comments
Post a Comment