Shabiki Gormahia Aibuka Na Jiwe Uwanjani
Baada ya wiki hii kusambaa kwa picha ya Shabiki wa Gor Mahia Winnie Nyar Kasagam zikimuonyesha akiwa na jiwe kubwa kwaajili ya kumpiga moja ya askari wa uwanja wa Kasarani 🇰🇪 hatimaye dada huyo amefunguka mkasa mzima ulivyokuwa
"Unajua Mimi ni mtu mtulivu sana, Winnie uliyemwona akibeba jiwe uwanjani hakuwa Winnie ambaye kila mtu anamjua,"
"Siku hiyo, nilichanganyikiwa kihisia, moyo wangu ulikuwa unauma. Na unajua, wakati wa maumivu ya moyo, akili na mwili hujibu.
"Mpenzi wangu alikuwa amevamiwa, Ilinikasirisha sana kwa sababu ananisaidia kifedha, na ndiye tegemeo katika uhusiano wetu.
"Mwanzoni, kulikuwa na tetesi kuwa ameuawa, hivyo nikatoka nyumbani hadi uwanjani kumuangalia mpenzi wangu Odinga, Nilipoingia uwanjani nikamkuta amelala chini amepoteza fahamu. .
"Hilo liliamsha hasira kali ndani yangu, mara moja, nilichukua jiwe kwenda kumtafuta mtu ambaye alimvamia mpenzi wangu"
"Nilipofika alipo, nilishtuka baada ya kugundua ni mtu ambaye nilimfahamu vizuri.
Binafasi najifahamu vyema nikiwa na hasira, Kwa hivyo nilidondosha jiwe hilo ili kuepusha kitendo ambacho ningefanya halafu nikaja kujutia baadae."
Tukio hilo lilitokea Februari 13 wakati Gor Mahia wakivaana na Vihiga katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Kenya 🇰🇪 ambapo mashabiki wachache walivunja geti wakitaka kutazama mechi hiyo bure na ndipo mpenzi wa dada huyo alipoadhibiwa na askari na kuumizwa.
Cc: Samuel
Comments
Post a Comment