Try Again tumezidiwa pointi 11, lakini tuna mechi 15 mbeleni
LICHA ya Yanga kutambia pointi 11 zaidi ilizoipiku Simba katika harakati za ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ ameonya wana mechi 15 watakazocheza kimkakati na wanaamini kushangaza wengi.
Amesisitiza
“Sawa tunaanza mzunguko wa pili tukiwa tumezidiwa pointi 11, lakini tuna mechi 15 mbeleni, hivyo tusubiri, msiwe na haraka na mambo”
Yanga Jumapili iliyopita ilifikisha pointi 42 na kujiimarisha kileleni kwenye msimamo ikiwapiku watani zao Simba kwa pointi 11 na kesho Wekundu wa Msimbazi wataikaribisha Biashara United ikiwa ni mechi yao ya kwanza ya mzunguko wa pili.
Hadi sasa Simba ni ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 31 na ikishinda itafikisha 34 na kupunguza gepu la pointi
Tofauti ya pointi hizo zimesababisha baadhi ya wapenzi wa Yanga kutamba
kasi hiyo haitoshuka kwenye mzunguko wa pili na kila timu ishinde mechi zake.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema “Pointi 11 hadi watufikie maana yake washinde mechi tatu na kutoka sare michezo miwili, wakati huo sisi tunafungwa, jambo ambalo wasilitarajie, Yanga hii ni moto mwingine.”
Jana Try Again alisema “Timu imerejea na tunaelekeza nguvu kwenye ligi kuendeleza safari yetu ya kutetea ubingwa, hii ni ligi sio mtoano, hivyo yeyote anaweza kufungwa na kushinda na kibao kikageuka wakati wowote.
“Sawa tunaanza mzunguko wa pili tukiwa tumezidiwa pointi 11, lakini tuna mechi 15 mbeleni, hivyo tusubiri kuona bingwa atakuwa ni nani mwishoni mwa msimu.”
Alisema msimu uliopita pia waliingia kwenye mechi za mzunguko wa pili wakiwa wameachwa kwenye msimamo, lakini kibao kiligeuka na kutwaa ubingwa.
Comments
Post a Comment