KAMA VIPI TUKUTANE kwa Mkapa, BERKANE YATIBUA MAMBO.
KAMA VIPI TUKUTANE kwa Mkapa, BERKANE YATIBUA MAMBO.
SIMBA ilipoteza mechi ya kwanza kwenye mechi za makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kunyukwa na RS Berkane kwa mabao 2-0, lakini ikajifariji kwa kusema itamaliza kazi Kwa Mkapa.
Simba ilikumbana na kipigo kwenye Uwanja wa Berkane, Morocco katika mechi ya Kundi D iliyopigwa kuanzia saa 4:00 usiku na kuifanya ing’oke kileleni hadi nafasi ya pili ikisaliwa na pointi 4 sawa na ilizonazo USGN ya Niger iliyoitoa nishai ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa kuilaza 2-0 katika mechi ingine ya kundi hilo.
Mabao mawili ya Adama Ba dakika ya 32 na Charki El Bahri dakika ya 41 yakitokana na makosa ya safu ya ulinzi ya Simba ilitibua rekodi ya Mnyama kundini.
Kocha Pablo Franco aliwaanzisha Nahodha John Bocco na Kennedy Juma badala ya Meddie Kagere na Yusuph Mhilu walioanza katika kikosi kilichovaana na USGN na kutoka nao sare ya 1-1 wiki iliyopita.
Berkane ilianza kwa kasi, japo kipindi cha pili Simba ilirudi kivingine baada ya mabadiliko ya kumuingiza Bernard Morrison badala ya Peter Banda na kuungana na Ousmane Sakho kuivuruga Berkane.
Simba sasa itakuwa na nafasi ya kulipa kisasi itakapoialika Berkane Machi 11 kwenye Uwanja wa Mkapa.
@mwanaspoti_tz
Comments
Post a Comment