Nimeamua Kuiza Chelsea Roman Abromavich

 Bilionea ambaye ni Mmiliki wa Club ya Chelsea ya England Roman Abramovich amethibitisha kuwa anataka kuiuza club hiyo ambapo anafanya hivi kwa maslahi mapana ya Club, Wadhamini na Wafanyakazi wa Club.


“Ningependa kutoa taarifa kuhusiana na tetesi zinazoendelea kwenye vyombo vya habari kuhusiana na umiliki wangu Chelsea, siku zote nimekuwa nikifanya maamuzi kwa sababu ya maslahi ya club, kwa hali inavyoendelea sasa nimeamua kuiuza club” ——— Roman Abromavich.


Roman aliinunua club hiyo 2003 kwa pound milioni 140 (Tsh Bilioni 433) na sasa ameamua kuiuza baada ya vita ya Ukraine kuisababishia Russia na Wawekezaji wake kuwekewa vikwazo au biashara zao kusitishwa sehemu mbalimbali.


Kwa mujibu wa Forbes Chelsea sasa ina thamani ya pound Bilioni 2.4 (Tsh Trilioni 7.4).


Roman katika taarifa iliyotolewa na Chelsea anasema atauza club hiyo na pesa zote alizouza zitaenda katika mfuko maalum wa kusaidia Waathirika wa vita nchini Ukraine na wala hana lengo la kujipatia Faida



Comments

Popular posts from this blog

Shafii Dauda Nipo Huru Sijafungiwa Na TFF

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes