KOMBE LA SHIRIKISHO CAF SIMBA SC WAHAHA


Leo Jumapili, Machi 20, 2022

.

ASEC MIMOSAS vs SIMBA SC

⏰ 19:00

🏟️ Stade de l'Amitié Cotonou Benin


Kinara wa kundi D Simba SC (pointi 7) atashuka katika dimba la Stade de l'Amitie kuchuana na wenyeji Asec Mimosas (alama 6) katika marudiano ya hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho. Huu ni mpambano muhimu ambao utaamua hatma ya kundi hili.

.

Baada kushinda 3-1 katika dimba la Benjamin Mkapa na kuvunja mwiko wa Asec Mimosas wa kutokufungwa, Simba SC itahitajika kuvunja mwiko mwingine wa Asec Mimosas wa kutokupoteza nyumbani.

.

WACHEZAJI WA KUCHUNGWA:

.

ASEC MIMOSAS

Kwa upande wa Asec Mimosas, chipukizi Karim Konate amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu akiwa amefumania nyavu mara 9 katika mechi 10 mpaka sasa.

.

SIMBA SC 🇹🇿

Mshindi mara mbili wa tuzo ya goli bora la wiki la #CAFCC Pape Sakho atakuwa alama ya kiulizo kwa kamati ya ulinzi ya Asec Mimosas.

.

Simba SC itawahitaji wachezaji wake wote kuwa katika ubora wao ikiwa inahitaji ushindi ili kukata tiketi ya robo fainali.

.

Asec Mimosas inahitaji ushindi ili kupanda kileleni mwa msimamo wa kundi D na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali.

.

Je, mnyama atapata alama 3 ugenini na kufuzu robo fainali?



Comments

Popular posts from this blog

Shafii Dauda Nipo Huru Sijafungiwa Na TFF

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes