CAF: SIMBA INAONGOZA KUTAZAMWA AFRIKA .
Kwa mujibu wa CAF, Simba imekuwa ndio klabu inayotazamwa kwa wingi na mashabiki kupitia akaunti za mitandao ya kijamii za CAF, ikiwamo Youtube (CAF TV) kulinganisha na timu nyingine kongwe Afrika na ikifuatiwa na Al Ahly ya Misri.
.
Rekodi zinaonyesha pambano lililotazamwa zaidi ni lile la Simba vs Al Ahly la msimu uliopita ambapo Simba ilishinda 1-0, kwani lilitazamwa na mashabiki zaidi ya milioni moja, huku maoni yakiwa zaidi ya 800.
.
Mechi iliyoshika nafasi ya pili ni Simba na AS Vita iliyopigwa Dar ikitazamwa na mashabiki 597,000 na ile ya ugenini ambayo Simba ilishinda bao 1-0 ina watazamaji 529,000 katika chaneli ya CAF TV.
Comments
Post a Comment