Posts

Showing posts from April, 2022

Familia Ya Mino Raiola Imetangaza Kifo Cha Mino Raiola

Image
 Wakala maarufu wa Wachezaji soka mbalimbali duniani kama Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic anayejulikana kwa jina la Mino Raiola amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 54, taarifa hizo zimethibitishwa na familia yake kupitia account yake ya twitter.

Cedric Kaze Simba Sc Ni Timu Bora

Image
 Kwanza kabisa, Sisi kama club tunajua umuhimu wa hii mechi na pia tunajua umuhimu wa kupata alama tatu kulingana na msimamo wa Ligi ili tuweze kuongeza tofauti na hii inatupa ari ya kujiamini na kuendelea kufanya vizuri zaidi kwenye Ligi. Pili, tunafahamu kabisa kuwa tunaenda kucheza na timu bora ambayo imetoka kucheza mashindano barani Afrika na kutolewa kwenye hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho, which is a very good achievement na wana wachezaji bora na wazoefu kwenye Ligi hivyo tuna amini utakuwa mchezo mzuri na nina ahidi sisi tutakuwa kwenye performance nzuri ili tuweze kupata alama tatu hapo kesho. Cedric Kaze, Kocha Msaidizi - Young Africans.

Kila Mtanzania Kupewa Gari Aina Ya NOAH

 ZIPO WAPI NOAH KWA KILA MTANZANIA?

RATIBA ya Michezo ya Leo Ijumaa April 29,2022

Image
 Tanzania – NBC Premier League 16:00 Geita Gold FC vs Azam FC ➡️England – Championship 21:45 Queens Park Rangers vs Sheffield United ➡️Spain – Laliga Santander 22:00 Sevilla vs Cadiz ➡️Germany – Bundesliga 21:30 Union Berlin vs Greuther Furth ➡️France – Ligue 1 22:00 Strasbourg vs Paris Saint-Germain ➡️Netherlands – Eredivisie 21:00 FC Utrecht vs NEC Nijmegen ➡️Portugal – Primeira Liga 22:15 Famalicao vs Estoril ➡️Belgium – First Division A: UECL Group 21:45 KRC Genk vs KV Mechelen ➡️Spain – Laliga Smartbank 23:00 Las Palmas vs Malaga ➡️Germany – 2. Bundesliga 19:30 FC Heidenheim vs Fortuna Dusseldorf 19:30 Hannover 96 vs Karlsruher SC 19:30 Sandhausen vs Schalke 04 19:30 St. Pauli vs 1. FC Nuremberg 19:30 Werder Bremen vs Holstein Kiel ➡️Netherlands – Eerste Divisie 21:00 ADO Den Haag vs Almere City FC 21:00 De Graafschap vs Jong PSV 21:00 FC Den Bosch vs Roda JC Kerkrade 21:00 FC Dordrecht vs FC Volendam 21:00 FC Eindhoven vs FC Emmen 21:00 Jong AZ Alkmaar vs Helmond Sport 21:00 ...

MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa April 29,2022

Image
  MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa April 29,2022

Mino Raiola Hajafariki Yupo ICU

Image
 πŸŽ™Kwa Mjibu wa mtu wa karibu wa  Mino Raiola, JosΓ© Fortes Rodriguez amekiambia chombo Cha habari Cha Uholanzi, Dutch media Kuwa Mino Raiola hajafariki dunia bali ana hali mbaya sana:  "Yupo kwenye hali mbaya,Lakini hajafariki dunia" (Source: @sgevans)

Taarifa mbaya Mino Raiola Afariki Dunia

Image
 Taarifa mbaya...  Mino Raiola amefariki dunia kutokana na maradhi.  Raiola ndio alikuwa wakala wa Erling Halaand, Zlatan Ibrahimovic, Paul Pogba pamoja na nyota wengine wengi.  RIP Mino Raiola πŸ’”

CEO wa klabu ya Simba sc Barbara Gonzalez awahusisha Yanga ishu ya Orlando Pirates

Image
 CEO wa klabu ya Simba sc Barbara Gonzalez awahusisha Yanga ishu ya Orlando Pirates. ▪️Amekanusha shutuma zote alizotoa kocha msaidizi wa Orlando Pirates Mandla Mcikazi kuhusu klabu ya Simba sc. ▪️Amesema media za Yanga zinatengeneza propaganda kuichafua Simba sc. ▪️ Barbara Gonzalez mesema, kocha Mcikazi anatafuta 'sympathy' kupalilia kibarua chake Orlando Pirates πŸ‡ΏπŸ‡¦ ▪️Amesema watatoa malalamiko yao rasmi kuhusu defamatory statements. πŸ” Lorenz Kohler Journalist πŸ‡ΏπŸ‡¦

Mwamnyeto Njia Panda Yanga Au Simba Sc

Image
 “Simba wanasumbua sana nisiseme uongo, wamekuwa wakiibuka na ofa kubwa kubwa.. ofa yao ni kubwa hasa ambayo nayo tumeamua kuichukua na kuendelea kuifanyia kazi" “Ukiacha Simba, Bakari ana ofa nyingi sana, kuna ofa tatu au nne hivi, kuna klabu ya Ugiriki, Malta na nyingine moja bado tunazungumza nazo.” •Meneja wa Mwamnyeto, Kassa Mussa-Via Mwanaspoti

Chico Ushindi Khali Tete Ndani Ya Yanga Sc

Image
 - Winga wa klabu ya Yanga Chico Ushindi amekuwa aki struggle kwa muda bila watu wengi kujua anasumbuliwa na nini. . . Kwa mujibu wa daktari wa ya Yanga sc Yousef Ammar πŸ‡ΉπŸ‡³ ameweka wazi kuwa Chico (26) πŸ‡¨πŸ‡© kwa vipindi tofauti alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya nyama za paja. . . Amesema wamelifanyia kazi suala hilo na sasa Chico ushindi amepona kwa 100% na yuko tayari kwa ajili ya michezo inayofuata.

Tutawachukulia Hatua Orlando PiratesBarbara Gonzalez Simba sc (CEO)

Image
 "Tutawachukulia hatua Orlando Pirates πŸ‡ΏπŸ‡¦ sio (CAF) pekee bali hata KIDIPLOMASIA, maneno waliyozungumza hayakubaliki. Hii si kwa Simba pekee bali kwa ajili ya Tanzania" πŸ” Barbara Gonzalez Simba sc (CEO)

ORLANDO PIRATES KUMKOSA DEON HOTTO DHIDI YA SIMBA SC.

Image
Wakati Kanoute na Onyango wakirejea Kikosini, Simba Sc wanatarajiwa kumkosa kiungo wao wa ushambuliaji Bernard Morisson kwenye mchezo ujao dhidi ya Orlando Pirates utakaopigwa Soweto wiki ijayo, Maharamia hao 'Orlando' nao watamkosa Deon Hotto baada ya kuoneshwa kadi ya tatu ya njano  itakayomfanya akose mchezo huo.

Orlando Pirates Media Zenu Zinadanganya

Image
 Povu la kocha wa Orlando Pirates baada ya Mchezo dhidi ya Simba sc kumalizika. "Media zenu zote hapa zinaenda kudanganya na kuandika uongo, semeni ukweli, Simba hakustahili kushinda" "Simba wamebebwa, hawajatutreat vizuri tangu tumefika, penati waliyopewa hawakustahili, VAR imewekwa lakini haijatumika katika maamuzi" . . "Kwa nini mnafanya haya kwa Waafrica wenzenu ? Je tutainua soka la Africa kwa namna hii ?! Na tunatoka hapa tukijisifu Simba kashinda, Simba hawajashinda referee ndiye amefanya Simba washinde" "Kama kweli Simba ni mabingwa wa kuhonga katika soka, ikibainika wanahonga mpaka waendesha (VAR) tutafika (CAF), mpaka (FIFA) tena wanaweza fungiwa mechi za Confederations of African Football (CAF)" . . "Mliyotufanyia hapa kuanzia Airport, Stadium hadi hotelini, Je mtafurahi tukiwafanyia haya pia mkija South Africa ? Tunarejea nyumbani kujipanga sisi hatutalipiza" . . πŸ” Mcikazi kocha wa Orlando Pirates akiongea kwa ukali na wana...

RIPOTI KUTOKA KWA MKAPA

Image
 RIPOTI KUTOKA KWA MKAPA. . FT: πŸ‡ΉπŸ‡Ώ SIMBA 1-0 ORLANDO πŸ‡ΏπŸ‡¦ ⚽️ Kapombe (pen) . Mechi ya Marudiano: πŸ—“ Jumapili, Aprl 24 πŸ‡ΏπŸ‡¦ Orlando Vs Simba πŸ‡ΏπŸ‡¦ Una neno lolote kuelekea mechi ijayo ya marudiano? NB:MAN OF THE MATCH INONGA BAKA.

Orlando Pirates Simba Sc Wametufanyia Fitina

Image
 Kocha wa klabu ya Orlando Pirates πŸ‡ΏπŸ‡¦ Mandla Nsikazi ameilalamikia klabu ya Simba sc kwa kuwapa pikipiki moja ya ESCORT katika jiji lililo na harakati nyingi na kupelekea kupata tabu njiani. . . Amesema mambo hayo watalipa nchini kwao South Africa πŸ‡ΏπŸ‡¦

KOCHA WA ORLANDO PIRATES: ADAI MAPOKEZI YALIKUA SIO MAZURI

Image
Mandla Ncikazi kocha wa Orlando Pirates akiongea na wanahabari na kuelezea maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba. Ncikazi amelalamika hawakupata mapokezi mazuri. Amedai hii sio mara ya kwanza kwao, wameshapitia vitu kama hivi. Asema Simba wakienda South watawapokea vizuri tu. Ameshangaa kwanini nchi nyingine za Afrika hazifanyi hivyo kama nchi yake. Kocha anasema wameifuatilia Simba, na amedai ni timu nzuri. Amewataja wachezaji kama Mugalu aliyewahi kucheza Zesco ya Zambia, Sakho anayetokea Senagal, Kagere, Mkude, Lwanga na mchezaji wao wa zamani Morrison. Amewagusia mabeki wa pembeni wa Simba ingawa hakuwataja majina. Amesema ni wazuri kwa kupanda mbele. Amegusia suala la Onyango kukosa mchezo wa kesho. Kocha amesema la muhimu kwao ni kucheza kwa kujiamini na kucheza kushinda mchezo wa leo.

Ni Simba Sc Vs Orlando Pirates Kwa Mkapa

Image
 -Leo klabu ya Simba SC inacheza mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup) dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini mchezo ambao utachezwa kuanzia majira ya saa 1:00 usiku kwenye dimba la Benjamini Mkapa.  -Simba wana kila sababu ya kushinda mchezo wao wa leo tena kuanzia magoli 2+ ili kuwe rahisi kufuzu nusu fainali ya kombe la shirikisho hadi fainali watanzania hawana budi ya kuiombea sana Simba Ili ipate ushindi wa kuanzia magoli mawili na kuendelea. Kila la Kheri Simba  Kila la kheri Tanzania

Orlando Pirates Kutua Dar Es Salaam Leo

Image
 nafahamishwa;  Orlando Pirates πŸ‡ΏπŸ‡¦ watawasili Dar es Salaam leo jioni kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Simba SC πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Jumapili.  Pia;  VAR ya mchezo huo itafungwa leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.  🚨

Orlando Pirates Kuwachunguza Simba Sc

Image
 Orlando Pirates πŸ‡ΏπŸ‡¦ wanafanya kila linalowezekana kupata matokeo chanya nchini Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ wiki ijayo.  Klabu hiyo ilipeleka baadhi ya mawakala kwenye mchezo wa Coastal Union dhidi ya Simba uliochezwa jijini Tanga.  Watatuma tena baadhi ya watu kutazama mechi dhidi ya Polisi leo.  Jumanne, kutakuwa na watu jijini Dar es Salam kupanga mahali pa kulala na kufanya mipango yote muhimu kabla ya timu kuwasili.