KOCHA WA ORLANDO PIRATES: ADAI MAPOKEZI YALIKUA SIO MAZURI

Mandla Ncikazi kocha wa Orlando Pirates akiongea na wanahabari na kuelezea maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba.


Ncikazi amelalamika hawakupata mapokezi mazuri. Amedai hii sio mara ya kwanza kwao, wameshapitia vitu kama hivi. Asema Simba wakienda South watawapokea vizuri tu. Ameshangaa kwanini nchi nyingine za Afrika hazifanyi hivyo kama nchi yake.


Kocha anasema wameifuatilia Simba, na amedai ni timu nzuri. Amewataja wachezaji kama Mugalu aliyewahi kucheza Zesco ya Zambia, Sakho anayetokea Senagal, Kagere, Mkude, Lwanga na mchezaji wao wa zamani Morrison.


Amewagusia mabeki wa pembeni wa Simba ingawa hakuwataja majina. Amesema ni wazuri kwa kupanda mbele. Amegusia suala la Onyango kukosa mchezo wa kesho.


Kocha amesema la muhimu kwao ni kucheza kwa kujiamini na kucheza kushinda mchezo wa leo.


Comments

Popular posts from this blog

Shafii Dauda Nipo Huru Sijafungiwa Na TFF

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes