Posts

Showing posts from May, 2022

Pablo Martin Out Simba Sc

Image
 -Klabu ya Simba SC imeachana rasmi na kocha mkuu wa klabu hiyo Pablo Martin raia wa Hispania baada ya kushindwa kufikia malengo ya msimu huu (2021/22). Uongozi wa juu wa klabu hiyo tayari umempa taarifa ya kuvunja mkataba wake pamoja na kocha wa viungo Don Daniel De Castro raia wa Hispania.

SASA RASMI MORRISON MALI YA YANGA SC

Image
Taarifa za kuaminika ni kuwa Mchezaji Benard Morrison yupo kwenye hatua za mwisho kumalizana na Yanga Inaelezwa kuwa Morrison alitakiwa kusafiri wiki hii kwenda kwao Ghana na uongozi wa Simba ulishafanya taratibu zote za kumkatia tiketi  Lakini katika hali isiyotarajiwa viongozi wa Simba wakimpigia simu Morrison kumuuliza kuhusu safari yake hapokei na wala hajibu msg  Katika hali ya kushangaza zaidi Afisa wa Simba aliyekua akimpigia simu Morrison alipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni Hajji akimuonya kuwa aache kumpigia Morrison  Afisa wa Simba aliendelea kumpigia Morrison na akapigiwa tena na mtu yule na kumueleza ujumbe ule ule kuwa aache kumsumbua Morrison  Imefahamika kuwa Morrison huenda akasafirishwa na Yanga kwenda Mwanza kushuhudia mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports  Taarifa za ndani ya Yanga zinaeleza kuwa viongozi wa Yanga wamegawanyika juu ya ujio wa Morrison ambapo wengi hawamtaki mchezaji huyo lakini mtu mmoja mwenye ushawishi kwa...

Kamati Ya Masaa 72 Uso Kwa Uso Na Jemedari Said Kazumari

Image
 -Kamati ya masaa 72 imeiomba mamlaka iliyomteua Jemedari Said Kazumari itengue uteuzi wa kuwa mjumbe wa kamati ya masaa 72 na imepeleka shauri lake kwenye kamati ya maadili kama kiongozi na mwanafamilia wa mpira wa miguu kutokana na kuandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akitumia picha za jongefu na mnato akitumia lugha kali  na yenye kushusha hadhi ya ligi kuu akitoa maoni yake kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Dodoma Jiji na Yanga SC kwa kusema kuwa ligi kuu ya NBC ni dhaifu.

Kisa Ambulance Namungo Wapewa Point Tatu Na TFF

Image
 -Klabu ya Namungo FC imepewa alama tatu na magoli matatu baada ya klabu ya Mbeya Kwanza kugomea mchezo namba 180 wa ligi kuu ya NBC kwa madai ya kutokuwepo kwa gari la wagonjwa (Ambulance) pia kocha wa timu hiyo Mbwana Makata na Meneja wa timu hiyo David Naftali wamefungiwa kujihusisha na soka kwa miaka mitano Kila mmoja kwa kushawishi wachezaji wasiingie uwanjani.

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Image
 -Mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM na mjumbe wa kamati ya usajili ya klabu ya Yanga Eng Hersi Said amekili kuwa wako kwenye mazungumzo ya kumsajili winga wa klabu ya Simba Benard Morrison raia wa Ghana mwisho wa msimu huu baada ya mkataba wake na Simba kuisha. Morrison tayari ameachana na Simba kwa kupewa mapumziko hadi mwisho wa msimu.

BREAKING NEWS!! Simba Sc Imeachana Na Bernard Morrison Rasmi

Image
BREAKING NEWS!! Klabu ya Simba SC imeachana rasmi na Mshambuliaji wao wa Kimataifa wa Ghana πŸ‡¬πŸ‡­,Bernard Morrison Baada ya kumpa likizo ya mda mrefu isiyo na kikomo mpaka Mkataba wake na Simba utakapoisha. AHSANTE na Kwaheri Mr Be....Umekaa Mda Mchache Tanzania....Lakini tumejifunza mengi kupitia wewe.

DTB Yamnasa Metacha Mnata Kutoka Polisi Tanzania

Image
 -Klabu ya DTB FC iliyopanda ligi kuu ya NBC imekamilisha usajili wa golikipa wa klabu ya Polisi Tanzania Metacha Mnata kwa mkataba wa miaka miwili. Metacha atajiunga na DTB mwisho wa msimu huu kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Polisi Tanzania kuisha.

Simba Sc Yakabidhiwa Milioni 50

Image
 -Klabu ya Simba leo imepokea zawadi ya fedha ya milioni 50 kutoka kwa mdhamini wao mkuu, kampuni ya Sportpesa kwa kufika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho (Caf Confederation Cup) barani Afrika

Simba Sc Kuachana Na Bernard Morrison

Image
  Uongozi wa juu wa klabu ya Simba SC umekubaliana kuachana na winga Benard Morrison raia wa Ghana mwisho wa msimu huu baada ya mkataba wake kuisha.

Simba Sc Kuachana Na Wachezaji Sita Wa Kimataifa

Image
 -Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba Kassim Dewji ambaye ni kaka yake na Mohamed Dewji tayari ametangaza kuisha kwa msimu wa 2021/22 kwa kushindwa kupata ubingwa wa ligi kuu na kushindwa kufika nusu fainali ya kombe la shirikisho.  -Kassim amesema tatizo kubwa lilikuwa washambuliaji wao msimu huu kutokuwa na makali kama misimu ya nyuma na msimu huu walitegemea sana viungo na mabeki kufunga magoli hivyo ametangaza kuwa watasajili washambuliaji wa nguvu kwa ajili ya msimu ujao. -Habari za uhakika kutoka Simba SC tayari walishamalizana na mshambuliaji wa Zanaco FC ya Zambia Moses Phiri na sasa wapo kwenye mchakato wa kukamilisha dili la mshambuliaji wa kimataifa wa Niger, Victorien Adebayor na wamepanga kuachana na wachezaji 6 wa kimataifa.

Kisa Vitochi FIFA Yaishushia Rungu Senegal

Image
 Shirikisho la soka Duniani (FIFA) limelitoza faini shirikisho la soka la Senegal kiasi cha Tsh (418) Milioni kwa kosa la mashabiki wa timu ya taifa ya Senegal πŸ‡ΈπŸ‡³ kuwamulika na tochi za laser Wachezaji wa timu ya taifa ya Egypt πŸ‡ͺπŸ‡¬ wakati wa mechi ya kufuzu kombe la Dunia 2022 iliyofanyika nchini Senegal πŸ‡ΈπŸ‡³ . . FIFA pia imewafungia kucheza bila mashabiki kwenye michezo inayofuata.

Ratiba ya Simba sc mwezi wa tano

Image
 Ratiba ya Simba sc mwezi wa tano ! ▪️03 = Namungo  -  Simba ▪️08 = Simba  -  Ruvu shooting ▪️11 = Simba  -  Kagera sugar ▪️14 = Simba  -  Pamba fc ▪️18 = Azam fc  -  Simba ▪️22 = Geita gold  -  Simba ▪️25 = Simba  -  KMC

Bernard Morrison Mikononi Mwa Police

Image
 -Mchezaji wa Simba SC Bernard Morrison raia wa Ghana anashikiliwa Kituo cha Polisi cha Chang'ombe kwakosa la kuwachoma na kitu chenye ncha kali mashabiki wawili wa Yanga na kumpiga shabiki mmoja wa Simba waliokuwa wanamzomea. -Morrison hakupanda Basi la timu baada ya mchezo kumalizika na badala yake alipanda gari yake ndogo kabla ya tukio kutokea. Inadaiwa kabla ya kupanda kwenye gari mashabiki walianza kumzomea, hivyo aliamua kuingia mbele kwenye gari ambapo alitoka na kitu kinachodaiwa kuwa ni bisibisi na kuwakimbiza mashabiki hao kisha kufanya vitendo hivyo.