Simba Sc Kuachana Na Wachezaji Sita Wa Kimataifa
-Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba Kassim Dewji ambaye ni kaka yake na Mohamed Dewji tayari ametangaza kuisha kwa msimu wa 2021/22 kwa kushindwa kupata ubingwa wa ligi kuu na kushindwa kufika nusu fainali ya kombe la shirikisho.
-Kassim amesema tatizo kubwa lilikuwa washambuliaji wao msimu huu kutokuwa na makali kama misimu ya nyuma na msimu huu walitegemea sana viungo na mabeki kufunga magoli hivyo ametangaza kuwa watasajili washambuliaji wa nguvu kwa ajili ya msimu ujao.
-Habari za uhakika kutoka Simba SC tayari walishamalizana na mshambuliaji wa Zanaco FC ya Zambia Moses Phiri na sasa wapo kwenye mchakato wa kukamilisha dili la mshambuliaji wa kimataifa wa Niger, Victorien Adebayor na wamepanga kuachana na wachezaji 6 wa kimataifa.
Comments
Post a Comment