Bernard Morrison Mikononi Mwa Police

 -Mchezaji wa Simba SC Bernard Morrison raia wa Ghana anashikiliwa Kituo cha Polisi cha Chang'ombe kwakosa la kuwachoma na kitu chenye ncha kali mashabiki wawili wa Yanga na kumpiga shabiki mmoja wa Simba waliokuwa wanamzomea.


-Morrison hakupanda Basi la timu baada ya mchezo kumalizika na badala yake alipanda gari yake ndogo kabla ya tukio kutokea. Inadaiwa kabla ya kupanda kwenye gari mashabiki walianza kumzomea, hivyo aliamua kuingia mbele kwenye gari ambapo alitoka na kitu kinachodaiwa kuwa ni bisibisi na kuwakimbiza mashabiki hao kisha kufanya vitendo hivyo.


Comments

Popular posts from this blog

Shafii Dauda Nipo Huru Sijafungiwa Na TFF

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes