SASA RASMI MORRISON MALI YA YANGA SC
Taarifa za kuaminika ni kuwa Mchezaji Benard Morrison yupo kwenye hatua za mwisho kumalizana na Yanga
Inaelezwa kuwa Morrison alitakiwa kusafiri wiki hii kwenda kwao Ghana na uongozi wa Simba ulishafanya taratibu zote za kumkatia tiketi
Lakini katika hali isiyotarajiwa viongozi wa Simba wakimpigia simu Morrison kumuuliza kuhusu safari yake hapokei na wala hajibu msg
Katika hali ya kushangaza zaidi Afisa wa Simba aliyekua akimpigia simu Morrison alipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni Hajji akimuonya kuwa aache kumpigia Morrison
Afisa wa Simba aliendelea kumpigia Morrison na akapigiwa tena na mtu yule na kumueleza ujumbe ule ule kuwa aache kumsumbua Morrison
Imefahamika kuwa Morrison huenda akasafirishwa na Yanga kwenda Mwanza kushuhudia mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports
Taarifa za ndani ya Yanga zinaeleza kuwa viongozi wa Yanga wamegawanyika juu ya ujio wa Morrison ambapo wengi hawamtaki mchezaji huyo lakini mtu mmoja mwenye ushawishi kwa Boss ndio anaengangania usajili huu.
Comments
Post a Comment