Posts

Pablo Martin Out Simba Sc

Image
 -Klabu ya Simba SC imeachana rasmi na kocha mkuu wa klabu hiyo Pablo Martin raia wa Hispania baada ya kushindwa kufikia malengo ya msimu huu (2021/22). Uongozi wa juu wa klabu hiyo tayari umempa taarifa ya kuvunja mkataba wake pamoja na kocha wa viungo Don Daniel De Castro raia wa Hispania.

SASA RASMI MORRISON MALI YA YANGA SC

Image
Taarifa za kuaminika ni kuwa Mchezaji Benard Morrison yupo kwenye hatua za mwisho kumalizana na Yanga Inaelezwa kuwa Morrison alitakiwa kusafiri wiki hii kwenda kwao Ghana na uongozi wa Simba ulishafanya taratibu zote za kumkatia tiketi  Lakini katika hali isiyotarajiwa viongozi wa Simba wakimpigia simu Morrison kumuuliza kuhusu safari yake hapokei na wala hajibu msg  Katika hali ya kushangaza zaidi Afisa wa Simba aliyekua akimpigia simu Morrison alipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni Hajji akimuonya kuwa aache kumpigia Morrison  Afisa wa Simba aliendelea kumpigia Morrison na akapigiwa tena na mtu yule na kumueleza ujumbe ule ule kuwa aache kumsumbua Morrison  Imefahamika kuwa Morrison huenda akasafirishwa na Yanga kwenda Mwanza kushuhudia mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports  Taarifa za ndani ya Yanga zinaeleza kuwa viongozi wa Yanga wamegawanyika juu ya ujio wa Morrison ambapo wengi hawamtaki mchezaji huyo lakini mtu mmoja mwenye ushawishi kwa...

Kamati Ya Masaa 72 Uso Kwa Uso Na Jemedari Said Kazumari

Image
 -Kamati ya masaa 72 imeiomba mamlaka iliyomteua Jemedari Said Kazumari itengue uteuzi wa kuwa mjumbe wa kamati ya masaa 72 na imepeleka shauri lake kwenye kamati ya maadili kama kiongozi na mwanafamilia wa mpira wa miguu kutokana na kuandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akitumia picha za jongefu na mnato akitumia lugha kali  na yenye kushusha hadhi ya ligi kuu akitoa maoni yake kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Dodoma Jiji na Yanga SC kwa kusema kuwa ligi kuu ya NBC ni dhaifu.

Kisa Ambulance Namungo Wapewa Point Tatu Na TFF

Image
 -Klabu ya Namungo FC imepewa alama tatu na magoli matatu baada ya klabu ya Mbeya Kwanza kugomea mchezo namba 180 wa ligi kuu ya NBC kwa madai ya kutokuwepo kwa gari la wagonjwa (Ambulance) pia kocha wa timu hiyo Mbwana Makata na Meneja wa timu hiyo David Naftali wamefungiwa kujihusisha na soka kwa miaka mitano Kila mmoja kwa kushawishi wachezaji wasiingie uwanjani.

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Image
 -Mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM na mjumbe wa kamati ya usajili ya klabu ya Yanga Eng Hersi Said amekili kuwa wako kwenye mazungumzo ya kumsajili winga wa klabu ya Simba Benard Morrison raia wa Ghana mwisho wa msimu huu baada ya mkataba wake na Simba kuisha. Morrison tayari ameachana na Simba kwa kupewa mapumziko hadi mwisho wa msimu.

BREAKING NEWS!! Simba Sc Imeachana Na Bernard Morrison Rasmi

Image
BREAKING NEWS!! Klabu ya Simba SC imeachana rasmi na Mshambuliaji wao wa Kimataifa wa Ghana 🇬🇭,Bernard Morrison Baada ya kumpa likizo ya mda mrefu isiyo na kikomo mpaka Mkataba wake na Simba utakapoisha. AHSANTE na Kwaheri Mr Be....Umekaa Mda Mchache Tanzania....Lakini tumejifunza mengi kupitia wewe.

DTB Yamnasa Metacha Mnata Kutoka Polisi Tanzania

Image
 -Klabu ya DTB FC iliyopanda ligi kuu ya NBC imekamilisha usajili wa golikipa wa klabu ya Polisi Tanzania Metacha Mnata kwa mkataba wa miaka miwili. Metacha atajiunga na DTB mwisho wa msimu huu kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Polisi Tanzania kuisha.