Shafii Dauda Nipo Huru Sijafungiwa Na TFF

 NIMEPOKEA ADHABU KWA MIKONO MIWILI.


"Nimeipokea adhabu ya kufungiwa, Taarifa ambayo imetajwa iliandikwa kwenye ukurasa wangu wa Instagram na ilikuwa inazungumzia u-dictator wa shirikisho"


"Kama unakumbuka, baada ya GSM kuingia mkataba na TFF, baadaye TFF wakaja na barua ikipiga marufuku wadau kuhoji kuhusu mkataba ule. Atakayethubutu atachukuliwa hatua"


"Baadaye GSM wakatoa barua ya kuvunja mkata na TFF. Baada ya hapo ndio likaandikwa andiko lililokuwa linazungumzia TFF kuzuia wadau kuhoji kuhusu masuala ya mkataba wao na GSM ambao baadaye GSM walitangaza kuuvunja"


"Kwa hiyo andiko langu lilikuwa linazungumzia kwamba TFF sio nyumba ya kupanga kwamba baba mwenye nyumba anaweza kuambua maji yatatoka muda fulani halafu bomba litafungwa"


"Unaweza kuwa umefungiwa lakini kumbe ndio upo huru zaidi! Hakuna vikwazo tena, kwa sababu hakuna vifungu vya kunizuia. Nitakuwa huru kuzungumza, kukosoa pale inapobidi ilimradi sivunji sheria". 


"Sasa hivi nahisi sijafungiwa ila ndio nipo huru. Nilikuwa kwenye kifungo cha miaka mitano (5) sasa hivi ndio nipo huru"


SHAFFIH DAUDA


Comments

Popular posts from this blog

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes