Yanga Sc Kuzindua Kadi Za Ki-Elekronic Leo

 Klabu ya Yanga SC hii leo itaweka rekodi ya kuwa Klabu ya kwanza Nchini Tanzania kwa Wanachama wake kutumia kadi za Ki-Elektroniki.


Uzinduzi wa Kadi hizo utafanyika kwenye Hotel ya Morena Jijini Dodoma ambapo Viongozi wa Yanga watakaohudhuria Ni CEO wao,Senzo Mazingisa,Katibu Mkuu wa Klabu hiyo,Haji Mfikirwa,Wakili Simon Patrick na Msemaji wa Yanga SC,Haji Manara.Mgeni rasmi Atakuwa Ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Tulia Ackson.


Yanga wamepanga kuwa kufikia Tarehe 30 March 2022 Matawi yote ya Klabu hiyo nchini yanatakiwa yawe yamehakiki Wanachama wake na kuhakikisha kila tawi lina Wanachama wasiopungua 100 kwa mujibu wa ibara 6(4) ya Katiba ya Yanga.


Lakini pia kufikia Tarehe 30 April 2022 Matawi yote yanatakiwa kuwa yamefanya uchaguzi kukidhi matakwa ya ibara ya 62(3) ya Katiba ya Yanga.


Baada ya hapo kuanzia May 2022 Mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanva utaanza rasmi na hapo ndipo wataenda kumchangua Rais wa Klabu hiyo.




Comments

Popular posts from this blog

Shafii Dauda Nipo Huru Sijafungiwa Na TFF

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes