Watu 13 Wapoteza Maisha Harusini
Sherehe moja ya harusi nchini India imeingia doa baada ya Watu 13 kuangukia ndani ya kisima na kufariki dunia, Mamlaka kutoka Jimbo la Uttar Pradesh zimethibitisha.
Waathirika ambao wote walikuwa ni Wanawake na Watoto, walikuwa wamekaa kwenye ubao uliofunika kisima ambapo ubao huo ulivunjija, Mtu mmoja amejeruhiwa kwenye tukio hilo.
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi amevitaja vifo hivyo kuwa vya kuhuzunisha moyo "Natoa pole nyingi kwa Familia za Marehemu na nawatakia majeruhi ahueni ya haraka"
Comments
Post a Comment