USGN Patachimbika Tu Simba Sc Tunajipigia Tu
USGN🇳🇪 wapinzani wa Simba SC kwenye mechi ya pili ya CAF Confederation Cup .
UNION SPORTIVE De La GENDARMERIE NATIONALE FOOTBALL CLUB ( USGN FC)
Union Sportive de la Gendarmerie Nationale ni klabu kutoka Niger yenye makao yake mjini Niamey🇳🇪.
🎯Iliundwa mwaka 1996 na inacheza ndani ya Ligi Kuu nchini humo Niger Premier League.✍️
Mwaka 2021 ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kombe la Ligi na kuwa mataji yao ya kwanza katika historia ya timu hiyo.✍️
🎯Wana uwanja wao wa nyumbani uitwao Stade Général Seyni Kountché wenye uwezo wa kubeba watazamaji 35,000✍️
🎯Wamecheza mechi nne (4) za CAF Champions League na mechi tatu (3) za CAF Confederation hawana historia kubwa kwenye soka.✍️
🎯Wana kikosi cha wachezaji 27 wenye wastani wa umri wa miaka 26. Wana wachezaji watano wanaocheza kwenye timu ya taifa.✍️
🎯kwa sasa wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi wakiwa alama 19 ndani ya mechi 10 walizocheza. Kinara ana alama 30 na amecheza mechi 12 ina maana USGN wana mechi mbili za viporo.✍️
Katika mechi hizo 10 za ligi wameshinda 5 sare 4 na kupoteza 1.
Thanks 😊🙏
@TotalEnergies CAF Champions League & Confederation Cup
Comments
Post a Comment