Shafii Dauda Afungiwa Na TFF Na Faini Juu

 -Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miaka mitano na faini ya sh. 6,000,000 (milioni sita) Shaffih Dauda ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kutoka Dar.


-Shaffih alilalamikiwa na Sekretarieti ya TFF kwa kutoa taarifa za uongo na kuchochea umma kupitia mtandao wake wa Instagram Februari 8, 2022 kinyume na kifungu cha 73(4)(a) pamoja na 75(5) vya Kanuni za Maadili za TFF, Toleo la 2021. Pia kwa kukiuka kifungu cha 3(1) cha Kanuni za Utii za TFF, Toleo la 2021.


Comments

Popular posts from this blog

Shafii Dauda Nipo Huru Sijafungiwa Na TFF

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes