Rais Samia Kuanzisha Kiwanda Cha Kuzalisha Chanjo Ya COVID-19
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kuzalisha chanjo za Covid 19 na maradhi mengine ndani ya Nchi kama njia moja ya kutimiza mipango ya Serikali ya kukabiliana na ugonjwa wa corona na magonjwa mengineyo.
Katika mazungumzo yake na Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel Brussels nchini Ubelgoji hapo jana, Rais Samia amesema Tanzania inataka kuwa muuzaji wa chanjo za kuokoa maisha kwa Jamii ya Afrika Mashiriki (EAC) na Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Rais Samia amesema bajeti ya Serikali ya Tanzania kununua chanjo inakadiriwa itaongezeka kutoka Tsh. Bilioni 26.1 mwaka 2020 hadi Bilioni 216 mwaka 2030 ambayo ni sababu maalum ya kujenga kiwanda hicho
‘’Tanzania inaomba kuwasilisha mapendekezo haya na natarajia mtawezesha wazo hili kuwa mradi wenye manufaa, nina amini, mpango huu ukitekelezwa, utafungua fursa mpya za kuimarisha uhusiano wetu zaidi"
#MillardAyoUPDATES
Comments
Post a Comment