Othman Kazi TUNAJUZANA KUHUSU VAR SYSTEM
Tupate Elimu kidogo kutoka kwa
Othman Kazi
TUNAJUZANA KUHUSU VAR SYSTEM
1. Gharama zake ni kiasi gani?
Kusimika mtambo wa VAR inagharimu £4.6M sawa na 14.5B Tsh.
2. Inaendeshwa chini ya chombo gani?_
VAR Huendeshwa chini ya IFAB International Football Association Board) (Bodi ya kimataifa ya shirikisho la soka)
3. Mtu Yeyote anaweza Oparate?_
Hapana, VAR ni mali ya IFAB, ina maana ukihitaji kusimika VAR nchini mwako utalazimika kuipata toka kwao tu.
4. Gharama za waendeshaji zikoje na nani analipia?_
Gharama za uendeshaji zipo juu sana hulipiwa na vilabu viwili husika vitakavyokuwa vinacheza siku hiyo, kwa mfano kuna mchezo wa FA cup kati ya Rochdale na Oxford United walijikuta wana bill ya £9251 (29M Tsh) pamoja VAT. Kwa kifupi hiyo bili hugawanywa kwa vilabu vyote viwili.Kwa ligi kama yetu kama utahitaji kulipia michezo yote 240 itabidi vilabu vitoe chini kidogo ya 7B Tsh kwa msimu
5. Kunahitajika nini ili kufanikisha uwepo wa VAR.
VAR huhitaji mazingira tulivu, kufanya kazi bila mihemko au mashinikizo ili iweze kutoa majibu yasiyo na shaka na yaliyo wazi. Huwa haiharakishwi kutoa majibu, lakini hupendeza kutoa majibu haraka ili kuwafanya wachezaji, makocha na mashabiki kutoingiwa na mihemko wakisubiri majibu.
🔸MAELEZO YA ZIADA
VAR system huweza kutumia camera 33 zilizo simikwa kwenye maeneo tofauti kwa mchezo mmoja, kwa baadhi ya viwanja England hutumia camera 38 na zote ni 5K zenye ubora wa picha wa hali ya juu kabisa kwa sasa duniani.
Katika hizo, camera 8 ni za (Super slow motion) mwendo wa pole na 4 ni za ultra slow motion) mwendo wa pole wa ziada.
Hii yote ni kumpa mwamuzi wa VAR wigo mpana wa kuona pande zote za tukio kabla ya kutoa maamuzi. Ligi tajiri Afrika kama PSL (South African soccer league) 🇿🇦 imeshindwa kuwa na VAR SYSTEM na sababu kubwa inayotolewa ni gharama kubwa za uendeshaji wake.
Salamu kwa Wanasiasa wa Tz, sisi tutengeneze tu Pitch kwanza za Viwanja Vyetu hili la VAR tujipe Mda kwanza
Comments
Post a Comment