Michezo Yaliyojiri Barani Ulaya Kwenye Magazeti
🚨 Karim Adeyemi na Dortmund wako katika makubaliano kamili kuhusu masharti ya kibinafsi ya kusainishana mkataba.
Dortmund wako tayari kutoa €30M + bonasi ya €5M lakini RB Salzburg wameomba ofa ya karibu €45M ili kumuuza mshambuliaji huyo.
(Chanzo: Sport1)
🚨 Kylian Mbappé amekataa ofa ya pili ya kandarasi mpya kutoka kwa timu yake ya PSG,
Kwa sasa Real Madrid wana uhakika watamsajili msimu huu wa joto bila malipo.
(Chanzo: @TheAthleticUK)
🚨 Cristiano Ronaldo anavutiwa vilabu vya PSG, Bayern Munich na Roma anapofikiria iwapo ataondoka Manchester United msimu huu wa joto.
(Chanzo: Sun Sport)
🚨 Harry Kane yuko tayari kuungana tena na Mauricio Pochettino huku kukiwa na ripoti kwamba meneja wa PSG atamlenga kama atakuwa kocha wa Manchester United.
(Chanzo: Daily Mirror)
Kylian Mbappé: kabla ya mechi ya jana
🗣️ "Watu wanazungumza kuhusu mimi na mustakabali wangu, ni jambo la kawaida - lakini kama mchezaji wa PSG, nitatoa kila nilichonacho. Ninaweza kuthibitisha kwamba mustakabali wangu bado haujaamuliwa - na mchezo huu na Real Madrid hautaweza. kubadilisha chochote,
(Chanzo : Fabrizio Romano)
Comments
Post a Comment