Mauwaji Kanisani Njombe

 Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe imetaja shauri namba 5 la mwaka 2022 linalowakabili Daniel Mwilango na Nikson Nyamideko wanaotuhumiwa kwa mauaji ya aliyekuwa Katibu wa Baraza la Walei Kanisa la Roman katoliki Kigango cha Parokia ya Makambako, Dickson Myamba (48) ambaye aliuawa kwa kukatwakatwa na mapanga katika duka lililopo ndani ya eneo la Kanisa.


Hakimu Mkazi Mfawidhi Matilda Kayombo amesema watuhumiwa Daniel Mwilango ambae ni Katekista (42) akishirikiana na Nikson Nyamwideko (23) wanadaiwa kuhusika na mauaji hayo February 7,2022.



Kesi imeahirishwa hadi February  28,2022 na Watuhumiwa wamerejeshwa rumande kutokana na kesi inayowakabili kutokuwa na dhamana.


Wawili hao wanadaiwa kumuua na kisha kumkatakata vipande Nickson Myamba  katika Mtaa wa Mangula Mjini Makambako huku chanzo kikitajwa kuwa ni chuki binafsi.

Comments

Popular posts from this blog

Shafii Dauda Nipo Huru Sijafungiwa Na TFF

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes