Maisha Ya Binadamu Yamejawa Na Changamoto Za Kihisia Na Mapenzi

 ."Mwanaume anaweza kuchepuka na bado akawa na upendo wa dhati kwa mke wake lakini Mwanamke hawezi kuchepuka na akaendelea kuwa na upendo wa dhati kwa mume wake" Nasema hv kwasababu mwanamume hafanyi tendo la ndoa kwa hisia,Mwanamke hawezi kufanya tendo la ndoa bila hisia MGUSO.Ndiyo maana wanaume wanahitaji mahali pa kufanya tendo la ndoa ila Wanawake wanahitaji sababu za kufanya tendo la ndoa. Wanawake wengi wanaoenda mahakamani kudai talaka kwa waume zao niwale WACHEPUKAJI, Mwanamke asiye chepuka hawezi kwenda mahakamani kudai talaka isipokuwa kama mume wake atakuwa amezidisha unyanyasaji wa kimwili na kiakili kiwango cha kukalibia kumuua mkewe.


Wanaume hawawezi kubadili tendo la ndoa na upendo.Mwanaume anaweza kufanya tendo la ndoa na Mwanamke lakini bado akawa hampendi-ndiyo maana wanawake wanaojikuta kwenye mahusiano ya kimapenzi na waume waliooa wanaowapenda wake zao kwa dhati hupata tabu sana kupata kufurahia mahusiano hayo kwani huwa wanatumika tu nahao wanaume wenye ndoa zao. lakini pindi tu mwanamke aliyeolewa anapolala na mchepuko wake huanza hata kusimulia habari za siri kuhusu mume wake na anaweza pia kusema nikwanamna gani anamchukia mme wake;anaweza hata kukubali kuchukua sumu kwa mchepuko wake ili amwangamize mme wake.


kwa Mwanaume tendo la ndoa na upendo ni vitu viwili tofauti kabisa, lakini kwa mwanamke tendo la ndoa na upendo ni vitu viwili vinavyo enda sambamba.kwa Mwanaume tendo la ndoa huja kwanza kabla ya upendo(MATAMANIO) lakini kwa mwanamke upendo huja kwanza kabla ya tendo la ndoa (upendo wa dhati) kwahiyo pindi mkeo anapo anza kuchepuka upendo wake huhama;anaweza hata kuanza kumpa chakula kizuri na mahaba ambavyo amekuwa akikupa ww tu.


Mwanaume akichepua haimaanishi kuwa ameacha kumpenda mkewe la hasha! ila siwezi sema hivyo kwa upande wa mwanamke.pindi mwanamke anapoanza kuchepuka anakuwa ametumbukia kimapenzi kwa mchepuko huo na maisha kwenye ndoa hayawezi kuwa sawa kamwe.


Comments

Popular posts from this blog

Tanesco Yashusha Neema Vijijini

Try Again tumezidiwa pointi 11, lakini tuna mechi 15 mbeleni