𝐑𝐔𝐕𝐔 𝐒𝐇𝐎𝐎𝐓𝐈𝐍𝐆 𝐇𝐀𝐖𝐀𝐍𝐀 𝐔𝐁𝐀𝐕𝐔 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐔𝐙𝐔𝐈𝐀

Meneja wa Simba Ahmed Ally amesema wako tayari kwa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa leo Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa


➪Baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Asec Mimosas katika mchezo wa kombe la Shirikisho, Ahmed amesema wataendeleza kasi yao mbele ya Ruvu Shooting hapo leo


➪"Tumetoka kula biriani, kawaida baada ya kula chakula kizuri unashushia na maji, juisi au soda sasa tunakwenda kushushia mchezo dhidi ya Ruvu Shooting"


➪"Tunajua mchezo hautakuwa mwepesi, mara nyingi unapocheza na timu za hapa nyumbani zinakamia, wote wanakaa nyuma kuzuia lakini naamini kwa moto tuliouwasha sasa, hawawezi kutuzuia kusonga mbele kwenye michuano hii," alitamba Ahmed


➪Simba itaikabili Ruvu Shooting ikiwa na kikosi chake kamili ambacho kitamjumuisha kiungo Clatous Chama ambaye alikosa mchezo uliopita wa Shirikisho dhidi ya Asec Mimosas


➪Pia winga Bernard Morrison amerejeshwa kikosini baada kumalizana na uongozi kuhusu tuhuma za utovu wa nidhamu


Comments

Popular posts from this blog

Shafii Dauda Nipo Huru Sijafungiwa Na TFF

Gsm Uso Kwa Uso Na Bernard Morrison

Chelsea Bango kubwa linasomeka kutoka Forbes